RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA MTOTO WA JAJI MKUU MJINI TANGA
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande
Othman kufuatia kifo cha mwanaye Said Mohamed Chande wakati Rais
alipokwenda Chumbageni Tanga kuhudhuria mazishi ya marehemu.
Jaji
Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman akiweka udongo katika kaburi la mwanaye
Said Mohamed Chande wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya
Chumbageni Tanga leo jioni.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Said
Mohamed Chande wakati ya mazishi yaliyofanyika katika eneo la
Chumbageni Tanga leo.Marehemu Said ni Mtoto wa Jaji Mkuu Mhe.Mohamed
Chande Othman.
Makamu
wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akiweka udongo katika kaburi la
mrehemu Said Mohamed Chande wakati wa mazishi yaliyofanyika huko
Chumbageni Tanga.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal,Jaji
Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman wakiomba dua wakati wa mazishi ya
marehemu Said Mohamed Chande ambaye ni mtoto wa jaji mkuu yaliyofanyika
katika makaburi ya familia huko Chumbageni Tanga leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Jaji Mkuu Mhe.Mohamed
Chande Othman(aliyesimama pembeni ya Rais) kufuatia kifo cha mwanaye
Said Mohamed Chande mjini Tanga.
(picha na Freddy Maro).
Comments
Post a Comment