MOTO WATEKETEZA MAROLI MAWILI YA MAFUTA MWANZA
Malori
mawili ya mafuta yameteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya
Jenereta iliyokuwa inatumika kushusha mafuta kutoka ndani ya malori hayo
kwa ajili ya kuyahifadhi kwenye kisima cha mafuta cha sasa kazi
kilichopo eneo la Butimba kona jijini Mwanza na kusababisha hasara ya
mamilioni ya shilingi,sambamba na kuteketea kwa pikipiki moja mali ya
Ayoub Ismail.

Muda
mfupi magari ya jeshi la zimamoto na uokoaji jijini Mwanza yakawasili
katika eneo la tukio yakiwa yamesheheni askari na kazi ya kuzima moto
huo ikaanza rasmi,huku baadhi ya wananchi waliofika mapema kushuhudia
tukio hilo wakieleza chanzo kilichosababisha malori hayo kushika moto na
kuteketea.
No comments:
Links to this post