Leo ninasherehekea siku yangu ya kuzaliwa na kwa namna ya pekee
ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki, kunishika mkono na
kuniongoza. Maisha yangu ni mfano wa baraka za Mungu. Kuna nyakati
nilianguka lakini
kwa upendo wake akaninyanyua na mpaka sasa ameendelea kunionyesha
baraka zake. Kwa namna ya pekee ninapenda kuishukuru familia yangu na
watanzania wenzangu kiujumla kwa upendo na imani yao juu yangu hata pale
nilipopitia vipindi vigumu katika maisha yangu. Nina furaha zaidi leo
kwa kuwa ninasherehekea siku yangu ya kuzaliwa nikiwa katika kilele cha
mapambano ya kusaidia wananchi wenzangu
Comments
Post a Comment