FILIKUNJOMBE APITA BILA KUPINGWA WAPINZANI WAKE WAINGIA MITINI NA FOMU ,MGOMBEA WA CHADEMA ASHINDWA KUJAZA TAREHE NA KUTORUDISHA FOMU MMOJA
fomu ya mgombea wa Chadema ubunge Ludewa zikiwa hazijatimia baada ya tomu ya tamko kukosekana
Fomu ya mgombea wa Chadema ikiwa haijazwa senemu ya tarehe ,mwezi na mwaka
Mzee Kada wa Chadema akimpongeza mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe baada ya kupewa barua ya kupita bila kupingwa
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Ludewa baada ya kupita bila kupingwa
Filikunjombe akionyesha barua ya kupita bila kupingwa
Msimamizi
wa uchaguzi jimbo la Ludewa Bw Wiliam Waziri akimpongeza mbunge
Filikunjombe baada ya kumkabidhi barua ya kupita bila kuingwa
ubunge jana
Na Matukiodaima Blog
ALIYEKUWA
mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) amepita bila
kupingwa baada ya mgombea wa chama cha Demokrasia na maendeleo
(chadema) Barthomew Mkinga kushindwa kutimiza Masharti na Taratibu za
Ujazaji wa Fomu.
Msimamizi
wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa Bw Wiliam Waziri alisema jana kuwa
Mgombea wa Chadema ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo
hivyo kukosa sifa ya kuwa Mgombea wa Ubunge hivyo kumkabidhi barua
rasmi Filikunjombe ya kupita bila kupingwa
Waziri alisema kwamba Kati ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni Mgombea wa CCM, Bw. Filikunjombe pekee;
Kuwa
Wagombea wa DP na TLP walishindwa kabisa kurejesha fomu huku Mgombea wa
Chadema akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha Fomu ya
Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi.
Mgombea
huyo wa Chadema aliyereja fomu ya wadhamini bila kujaza tarehe
,mwezi wala mwaka ambao uchaguzi mkuu utafanyika .
Kwa
upande wake mgombea ubunge wa TLP Bw Blanka Haule alisema kuwa
alishindwa kurejesha fomu hizo kwa wakati kutokana kukosa picha za
kubandika katika fomu hiyo kutokana na hali ya mazingira ya Ludewa
kukowa eneo la kupiga picha hizo.
Kwani
alisema picha ambazo alipiga Njombe alizisahau alikoziweka hivyo
kulazimika kwenda kupiga pich nyingine za haraka kwa muda wa
dakika tatu ila cha kushangaza dakika tatu za kutoka picha hizo
zilionekana kushindwa kutoka kwa wakati na kutoka saa 11 jioni .
“Nilijipanga
kugombea ubunge ili kumpokea ubunge Deo Filikunjombe na
kuendeleza yale yote aliyoyafanya jimboni ila watu wa picha
walinikwamisha na kushindwa kupata picha kwa wakati hivyo kwa sasa
ndio basi tena japo ilikuwa ni Demokrasia lakini kapita bila
kupingwa ndio mbunge wetu:”
Akizungumzia
hatua ya mgombea wao wa Chadema kushindwa kukamilisha taratibu
za ujazaji wa fomu hizo Bw Daniel Songo alisema kuwa mgombea wao
hakuwa makini hata kidogo kwani alikuwa ni mtu ambae hakutulia na muda
mwingi alikuwa akifikiria juu ya wanachama wanaohama chama na
kuacha kutulia katika kujaza fomu hizo .
Japo
alisema chama hicho kimepoteza umaarufu kutokana na mwenendo wa
viongozi wa juu wa chama hicho kuendekeza siasa za ukanda zaidi na
kuacha kutazama uhai wa chama hicho.
Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Ludewa Stanle Kolimba alisema kuwa amepokea kwa
furaha kubwa hatua ya mgombea wake wa nafasi ya ubunge kupita bila
kupingwa na kuwa kazi kubwa kwa sasa kuhakikisha mgombea urais wa CCM
Dr John Magufuli anapata kura za kimbunga pamoja na kupigania kata
zote kuona CCM .
Kwa
upande wake Bw Filikunjombe akizungumzia hatua hiyo ya kupita bila
kupingwa alisema ameipokea kwa vizuri sana kwa alitegemea wapinzani
hao wajitokeze ili aweze kuwaonyesha kazi kwa kuhakikisha
wanaangukia pua katika uchaguzi huo .
Alisema
kazi kubwa ya maendeleo ambayo ameifanya katika jimbo hilo kwa miaka
mitano na imani kubwa ambayo wananchi wa Ludewa wanayo dhidi yake
ilikuwa ni vigumu kwa wapinzania hao kupata kura Ludewa.
Bw
Filikunjombe aliwaomba wananchi wa Ludewa kura zote ambazo
walipanga kumpigia yeye kuzielekeza kwa mgombea Urais Dr Magufuli na
kwa madiwani wa CCM na furaha yake kuona wapinzani wanaambulia
patupu katika wilaya ya Ludewa
Comments
Post a Comment