ASKOFU ABAKA MWANAFUNZI HUKO SHINYANGA...HIKI NDICHO KILICHOMKUTA!
Askofu wa Kanisa la Tanzania Field Evangelism (TFE) la mkoani Shinyanga, Edson Simon.
Mashaka
Baltazar, MwanzaDunia imekwisha na kama mti mbichi unatenda haya
itakuwaje kwa mti mkavu? Askofu wa Kanisa la Tanzania Field Evangelism
(TFE) la mkoani Shinyanga, Edson Simon, amehukumiwa kwenda jela miaka 30
baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji wa mwanafunzi katika kesi
iliyokuwa ikimkabili.
Askofu
Simon alihukumiwa kifungo hicho Agosti 14, mwaka huu na Hakimu wa
Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mkoani hapa, Martha Mpanze baada ya
kujiridhisha na ushahidi wa upande wa mashitaka.
Habari
zilizopatikana mahakamani hapo zilieleza kuwa, hukumu hiyo ilisomwa na
Abesizya Kalegeya kwa niaba ya Hakimu Mpaze aliyeisikiliza kesi hiyo na
kuandaa hukumu hiyo.
Akisoma
hukumu hiyo, Kalegeya aliiambia mahakama hiyo kuwa, kulingana na
ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, ulithibitisha mshitakiwa
alitenda kosa hilo, kinyume na kifungu cha 130, kifungu kidogo (1) na
(2)(e) na 131 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Ilielezwa
kuwa, Kalegeya aliiambia mahakama hiyo kuwa, Askofu Simon alitenda kosa
la ubakaji miezi kadhaa iliyopita kinyume cha sheria ya makosa ya
kujamiiana baada ya kumwingilia mwanafunzi wa kike wa shule moja ya
sekondari iliyopo wilayani Magu (jina tunalo) mwenye umri wa miaka 16
(jina linahifadhiwa kimaadili).
Habari zilieleza kwamba, kutokana na kosa hilo, mahakama hiyo ilimtia hatiani Askofu Simon na kumhukumu kwenda jela miaka 30.
Katika
kesi hiyo ambayo Askofu Simon alikuwa akitetewa na wakili wa
kujitegemea, Anthony Nasimire, mtumishi huyo wa Mungu alidaiwa kumbaka
denti huyo ambaye alikwenda kuombewa kanisani kwake.
Ilielezwa
kuwa, katika hati ya mashitaka, maelezo yalionesha kwamba mwanafunzi
huyo aliwahi kuishi nyumbani kwa askofu huyo, kabla ya kusafiri naye
hadi katika hoteli moja jijini hapa iliyopo Mtaa wa Rufiji ambapo
alidaiwa kumwingilia kwa siku kadhaa.
Comments
Post a Comment