WATUHUMIWA WA UJAMBAZI STAKISHARI WATIWA MBARONI



Kituo cha Polisi Stakishari kilichovamiwa na majambazi.
JESHI la Polisi jijini Dar es Salaam limewakamata watu watano waliohusika na tukio la ujambazi katika Kituo cha Stakishari, kilichopo Ukonga jijini Dar pamoja na silaha kadhaa.
Katika tukio hilo bunduki aina ya SMG 7, SAR 7 na risasi 28 za SMG vimekamatwa vyote vikiwa vya Kituo cha Stakishari. Mbali na vitu hivyo, sanduku lenye fedha kiasi cha shilingi milioni 170 pamoja na pikipiki 4 vimekamatwa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, ameapa kwamba Jeshi hilo litawakamata wote waliohusika na tukio hilo, pia amesema kama wapo watu waliohusika na tukio hilo wajisalimishe mapema.

Comments

Popular posts from this blog