UZINDUZI RASMI WA KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI NI KESHO VIWANJA VYA MWEMBE YANGA JIJINI DAR ES SALAAM MAANDALIZI YAMEKAMILIKA WANA MUZIKI LULUKI KUTOA BURUDANI WANDUGU SAIDIA TUTANI UZINDUZI RASMI NI KESHO

 Mshauri wa masuala ya Malaria kutoka Taasisi ya Jhpiego, Jasmin Chadewa (kushoto), akitoa huduma ya kumpa dawa ya vitamini A, mtoto Rahim Simai,  viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi ikiwa ni utoaji huduma wa elimu ya afya kwa wajawazito na matumizi ya dawa aina ya SP, upimaji wa malaria pamoja na matumizi ya vyandarua kama muendelezo wa huduma za afya ya mama mjamzito na mtoto kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili wa Kampeni ya Wazazi Nipendeni utakaofanyika kesho katika viwanja hivyo.
 Wakina mama wakisubiri kupata huduma katika moja ya banda yaliyopo viwanja vya Mwembe Yanga.
 Maofisa Taasisi ya Center for Comminication Programs Johnns HopKins University wakifunga kitanda cha kujifungulia wajawazito wakati wakitoa huduma mbalimbali viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi tayari kwa uzinduzi wa Kampeni ya Wazazi Nipendeni utakaofanyika katika viwanja hivyo kesho.
Mtaalamu wa Maabara Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Mbwana Mohamed (katikati), akimtoa damu, Juma Bakari mkazi wa Yombo Kilakala ikiwa ni utoaji huduma kuelekea uzinduzi wa Kampeni ya Wazazi Nipendeni utakaofanyika kesho. Katikati ni Maida Millanzi wa Hospitali hiyo.
Maofisa Taasisi ya Center for Comminication Programs Johnns HopKins University wakifunga chandarua katika utoaji wa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi.
Msimamizi wa masuala ya Malaria  Kata ya Kurasini Hondo Mwindeni (wa pili kulia), akiwaelekeza wananchi waliotembelea moja ya banda jinsi ya kujikinga na vidudu vya malaria.
Mtaalamu wa Maabara Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Mbwana Mohamed akimtoa damu mpiga picha wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Abdallah Kaniki kwa ajili ya kumpima malaria.
Burudabni mbalimbali zikiendelea. Lakini kesho katika viwanja hivyo itakuwa ni zaidi ya burudani.

Dotto Mwaibale

BENDI ya muziki wa dansi nchini, FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma'
wanatarajia kutoa burudani  ya nguvu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya 'Wazazi Nipendeni', itakayofanyika leo kwenye viwanja vya
Mwembe Yanga wilayani Temeke jijini , Dar es Salaam.

Mbali na bendi hiyo kutumbuiza leo, pia kutakuwa na uhondo
mwingine utakaotolewa na wasanii wa kizazi kipya nchini Chegge
Chegunda, Mh Temba na Juma Nature. 

Akizungumza Dar es Salaam jana kiongozi wa FM Academia, Nyoshi el Sadaat alisema watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi, ili kujua jinsi ya kujikinga na maambukizi pamoja na kumlinda mama na mtoto huku  wakipata burudani kali toka kwetu bure.

Alisema kuwa nyimbo zote zitakazoimbwa katika viwanja hivyo, zitakuwa na ujumbe utakaogusa watu wa rika zote.

Kiongozi huyo alisema licha ya kupiga nyimbo hizo zitakazokuwa na
ujumbe utakaowagusa wa watu rika zote kutokana na maambukizi, pia
watapiga nyimbo zao zilizowahi kutamba na zinazotamba sasa.

"Tutaporomosha nyimbo zetu zote kali zikiwemo Heshima kwa wanawake, Anna, Sumbungengi, Prison, Kazi ni kazi na nyingine nyingi ambazo tunaamini zitakuwa burudani tosha kwa mashabiki wa dansi watakaofika viwanja vya Mwembe Yanga," alisema Nyoshi

Nyoshi alisema hii itakuwa ni mara ya pili kushiriki kampeni yenye
maudhui kama hayo, hivyo hatowaangusha katika upande wa
burudani."Kundi letu limejipanga vizuri na tutahakikisha ujumbe
tutakaoutoa siku hiyo utabadilisha mwenendo wa jamii ya Tanzania na
kujua thamani zaidi ya kumlinda mama na mtoto," alisema Nyoshi.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi huo wa Wazazi Nipendeni, Waziri Nyoni  alisema kila kitu kimekamilika kuhusiana na tamasha hilo na pia utoaji wa elimu kuhusu Afya ya mama na Mtoto inaendelea kwa siku zote mbili jana na leo.

“Elimu ya afya ya mama na mtoto ni muhimu hivyo tunawakaribisha
watanzania wote mje kupata burudani na elimu ya afya ya mama na mtoto.

Alisema kufayika kwa Kampeni ya Wazazi Nipendeni ni ya awamu ya pili kwa udhamini wa  shirika la Maendeleo ya Kimataifa la watu wa Marekani (USAID),  ikiwa kwa lengo la kumwezesha mjamzito na mwenza wake kuchukua hatua muhimu kuwa na maendeleo mazuri ya ujauzito, kujifungua salama na kuwa na mtoto mwenye afya njema, hadi anapofika mwaka mmoja,” alisema. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

Comments

Popular posts from this blog