RAIS JAKAYA KIKWETE KUWA MGENI RASMI KUMBUKUMBU YA MASHUJAA
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa
zitakazofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam.Bw. Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi
Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana, pia
wananchi watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia
matukio yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa
zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja.
Askari
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi
katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu
ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.Picha na
Aron Msigwa.
RAIS JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA!
Na.Aron Msigwa - MAELEZO.
23/7/2015. Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete anatarajia kuwa
mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa
itakayofanyika Julai 25, 2015 Katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es salaam.
Akizungumza
mara baada ya kukamilika kwa maandalizi ya maadhimisho hayo leo jijini
Dar es salaam,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki amesema
maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam kuwakumbuka na
kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga kupigania uhuru na ukombozi wa
Taifa la Tanzania,kulinda na kudumisha amani na utulivu wa nchi.
Amesema
Maadhimisho hayo yatapambwa na Gwaride la Kumbukumbu litakaloandaliwa
na vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi ,Magereza na
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Aidha,
amesema kutakuwa na Mizinga salama itakayopigwa, uwekaji wa silaha za
asili na maua kwenye mnara wa kumbukumbu, Kutakuwa na sala na Dua
kutoka kwa viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya dini hapa nchini.
Bw.
Sadiki amefafanua kuwa shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja
zitaanza saa mbili Asubuhi na kumalizika saa sita mchana ambapo wananchi
watakaohudhuria kumbukumbu hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio
yatakayokuwa yananendelea uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa
zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya uwanja.
Ameongeza
kuwa siku hiyo baadhi ya barabara katika jiji la Dar es Salaam zikiwemo
Lumumba ,Uhuru na Bibi Titi zitafungwa kwa muda ili kuhakikisha
usalama wa watumiaji wa barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho hayo .
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa ufafanuzi kuhusu
changamoto zinazoendelea kujitokeza za kusuasua kwa zoezi uandikishaji
wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa BVR
jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment