MAKONDA AZINDUA KISIMA CHA MAJI SAFI KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA WATOTO WETU TANZANIA KILICHOJENGWA NA KAMPUNI YA SIMU YA ZANTEL
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (katikati), akimkaribisha Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati akiwasili kwenye hafla ya
kuzindua kisima cha maji safi katika Kituo cha Watoto Yatima cha Watoto
Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana.
DC Makonda akisaini katika kitabu cha wageni katika kituo hicho.
Mmoja wa vijana wa kituo hicho akiigiza igizo kuonesha changamoto zinazowakabili watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu
Tanzania, Evans Tegete (kulia), akizungumza katika hafla ya kuzindua
kisima hicho. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya
Zantel, Pratap Ghose na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Naibu Mkurugenzi wa Kituo
hicho, Theobard Bubelwa (kulia), akiteta jambo na Chief Commerial
Officer wa Zantel, Sukwinder Bajwa wakati wa hafla hiyo.
Watoto wa kituo hicho na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Watoto wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akipokea risasi ya watoto wa kituo hicho.
Vijana wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alitoa ahadi ya kuwasomesha baadhi ya wanafunzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Paul Makonda, akifungua pazia wakati akizindua kisima cha maji katika
Kituo cha Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es
Salaam jana. Kisima hicho kimejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Simu ya
Zantel.
DC Makonda akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa kisima hicho.
Hapa DC Makonda akimtwisha maji mmoja wa wanafunzi wa kituo hicho baada ya kukizindua.
DC Makonda akimkabidhi kitabu, mtoto Yusla Omari kwenye uzinduzi huo.
DC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya kituo hicho.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Simu ya Zantel jana ilitoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto
yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza
tatizo la maji na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa
takribani watoto 70 wa kituo hicho.
Tatizo la maji ni moja ya matatizo sugu
katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla hivyo msaada
huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho.
Kisima hicho kilichokabidhiwa jana
kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa matumizi ambayo
yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na maambukizi
ya maji yasiyo salama na machafu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ,
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni
ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu kwa wateja
wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii
na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka
‘Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya
wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu wa
kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza moja ya matatizo
yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu’ alisema Pratap.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika shughuli ya makabidhiano
hayo, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada huo akisema ni ishara
inayofaa kupongezwa.
‘Ustawi wa watoto na vijana ni jambo
muhimu katika jamii, hivyo nakipongeza kituo hiki kwa kazi kubwa
wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu
katika jamii, na ninatoa wito kwa makampuni mengine kushiriki na
kusaidia kituo hiki’ alisema Makonda.
Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo
Mbezi Suka jijini Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2001, kwa lengo la
kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu
bora.
Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Kituo
cha Watoto Wetu Tanzania,Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa na
tatizo kubwa la maji, lakini sasa shukrani kwa Zantel tatizo hilo
limemalizika.
Comments
Post a Comment