BREAKING NEWS : LOWASSA ATAJA SIKU RASMI YA KUAMIA CHADEMA
Zipo tetesi kwamba Edward Lowasa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya
ufisadi wa Richmond anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari
Jumapili tarehe 26 Julai 2015 Jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo,
Lowasa anatarajiwa kueleza mambo mengi juu ya mchakato wa uchaguzi ndani
ya CCM uliopelekea jina lake kukatwa.
Pia katika mkutano huo, Lowasa anatarajiwa kutangaza rasmi kujivua
uanachama wake ndani ya CCM na kujiunga na CHADEMA ambapo baadaye jioni
ataelekea viwanja vya Mwembeyanga ambako ataungana na viongozi wengine
wa CHADEMA kwenye mkutano wa hadharaza. Mtakumbuka kuwa uwanja huo wa
Mwembeyanga uliopo Temeke Dar es Salaam ulitumika kutaja orodha ya
mafisadi 11 na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa mwaka 2007 ambapo
jina la Lowasa lilikuwa miongoni mwa majina yaliyopo kwenye orodha hiyo.
Uamuzi wa Lowasa kwenda CHADEMA umetokana na kutimiza makubaliano ya
kupeleka shilingi bilioni 10 ambapo fedha hizo zimekabidhiwa Jana
Alhamis Tarehe 23 Julai 2015. Aliyekabidhi fedha hizo kwa Mwenyekiti wa
CHADEMA, Freeman Mbowe ni Apson Mwang'onda na makabidhiano yamefanyika
kwenye Hotel ya Sea Cliff huku tukio hilo likishuhudiwa na Kingunge
Ngombale Mwiru na wengine ambao sitawataja kutokana na sababu maalum.
Taarifa zinasema kuwa kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa watu
walioathirika na kukatwa kwa Lowasa hasa kutokana na fedha nyingi na
muda kwa matumaini kuwa watakuwa "UPPER" baada ya Lowasa kushinda Urais.
Miongoni mwao ni pamoja na Prof Juma Kapuya, Nazir Karamagi, Parseko
Kone, Mgana Msindai, Kingunge Ngombale Mwiru, Mchungaji Gwajima, Andrew
Chenge nk.
Hata hivyo, inadaiwa pia kuwa watu walio karibu na Lowasa akiwemo
mfadhili wake mkuu Rostam Aziz ambaye amegoma kutoa fedha za kufadhili
harakati za kwenda upinzani wanaendelea kumsihi kuwa asiende huko kwani
atakuwa amejimaliza kabisa kisiasa. Pia inadaiwa kuwa mkewe Regina
Lowasa amekuwa bitter sana na mpango wa mumewe kwenda upinzani na kwamba
kwa siku kadhaa sasa amekuwa akiwafukuza wageni waliokuwa wanaenda
nyumbani kwake hasa wale wa upinzani.
Hata hivyo, uamuzi wa Lowasa kwenda CHADEMA unatokana na msukumo wa
maslahi binafsi baina ya Lowasa, Freeman Mbowe na wale waliomzunguka
Lowasa na kwamba mpango huo ni hatari kubwa kwa ustawi wa CHADEMA.
FREEMAN MBOWE anamtaka Lowasa kwa tamaa ya fedha ambapo matamanio yake
yamekamilika baada ya kukabidhiwa shilingi bilioni 10 alizohitaji. Hata
hivyo, upo uwezekano kuwa fedha hizo zikamtokea puani hasa pale
atakaposhindwa kushawishi viongozi wa UKAWA kumteua Lowasa kupeperusha
Bendera yao kwa mujibu wa makubaliano ya Lowasa na Mbowe.
Pia mtakumbuka kuwa Lowasa ameenguliwa CCM kutokana na kukiuka kanuni na
taratibu za chama huku kashfa za ufisadi zikitumika kama kigezo kikuu
cha kuenguliwa kwake. Lowasa huyu anayeenda CHADEMA ni Lowasa yule yule
wa Kashfa za Richmond na kwamba CHADEMA wanapokea mtu ambaye taifa
limemkataa.
Aidha, viongozi wa CHADEMA wamekuwa na kauli tofauti juu ya Lowasa huku
Tundu Lissu na Wilbroad Slaa bila kumsahau Godbless Lema wakiongoza
mashambulizi dhidi ya Lowasa. Mathalan, hotuba za viongozi hawa wakati
wa Uchaguzi Mdogo wa Arumeru Mashariki ambapo Nassari alikuwa anapambana
na Sioi Sumari, Mkwe wa Lowasa zilitawala kashfa za Lowasa na kashfa
hizo ndizo zilizopelekea Nassari kushinda. Pia, Dr Slaa amemtaja Lowasa
kwenye list of shame na hajajitokeza kwenye vyombo vya habari na
kutangaza kuwa amemuondoa kwenye Orodha hiyo.
Vilevile, shinikizo la Lowasa kwenda CHADEMA linafanywa na watu ambao
image yao kwenye public ni mbaya. Watu kama Prof Kapuya, Nazir Karamagi,
Andrew Chenge na wengineo hakika wanawakilisha kikundi cha watu ambao
hawana taswira nzuri kwenye jamii.
CHADEMA wana wakati mgumu sana katika kumnadi Lowasa. Siku zote wamekuwa
wakijipambanua kuwa chama chao kinapambana na ufisadi. Inashangaza kuwa
wanaojinasibu kuwa wanapambana na ufisadi ndo wanapokea rushwa na
wanakaribisha mafisadi kwenye chama chao.
Natambua kuwa CHADEMA wanataka kumtumia tu Lowasa katika uchaguzi Mkuu
ujao na baada ya hapo watamtema. Hata hivyo watambue kuwa uamuzi huo si
tu utakuwa na athari kwa Lowasa bali hata wao CHADEMA watakuwa
wamejimaliza.
Nimalizie kwa kusema kuwa Lowasa huyu ambaye ameonekana mchafu ndani ya CCM hawezi kuwa msafi ndani ya CHADEMA.
CHANZO FULL HABARI
CHANZO FULL HABARI
Comments
Post a Comment