Skip to main content
MTITU, STEVE NYERERE BIFU KALI WAAPA KUTOZIKANA!
Msanii
wa filamu Steven Mengere ‘Steve Nyerere’. Wakizungumza na Amani kwa
nyakati tofauti juzi, wawili hao wameapa wasijuane kwa hali yoyote iwe
kwa matatizo kama mmoja wao kufiwa au yeye kufariki dunia, basi mwingine
asihudhurie msiba na mazishi. WASANII William Mtitu na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wamejiapiza kuwa
wasizikane ikitokea mmoja kati yao akafariki dunia huku chanzo ni kila
mmoja kumtuhumu mwenzake kwa unafiki.
Steve
Nyerere, ndiye alikuwa wa kwanza ‘kuachama’ mbele ya gazeti hili ndani
ya Viwanja vya Leaders, Dar kulikokuwa na kikao cha maandalizi ya
sherehe ya harusi ya msanii mwenzao, Hadji Adam ‘Baba Haji’.
“Hakuna
mtu mnafiki kama Mtitu, sitaki kabisa hata kumsikia na kila nikimtazama
najisikia vibaya mno, mkiwa pamoja anaonekana mwema lakini baada ya
hapo anakuwa msaliti, kwanza hata nikifiwa sitaki kumuona msibani,
nikifa mimi hakika asihudhurie mazishi yangu, naapa,” alisema Nyerere
huku akimtazama mwandishi kwa jicho la ‘sitanii kaka’.
Naye kwa upande wake, Mtitu aliposikia hayo alionekana kumpuuza Nyerere huku akimtolea maneno ya kejeli na dharau tele.
Msanii
wa filamu William Mtitu. “Steve ni mtoto mdogo sana halafu hana elimu
kichwani, ameingia kwenye sanaa tunamuona, hana jipya zaidi ya
kujipendekeza kwa viongozi wa serikalini kwa kuwaomba hela. Atafute mtu
wa kushindana naye. Hata mimi nikifa asikanyage msibani na kaburini
kwangu, nitazikwa hata na mawe au wanyama,” alisema Mtitu kwa sauti
iliyojaa jazba
Comments
Post a Comment