JOHARI: RAY NI KILA KITU KWANGU!
PATAMU
hapo! Diva wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema msanii
mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ ndiye kila kitu maishani mwake kutokana
na msaada aliompa wa kumtoa kisanii na kumsapoti kwa mambo mengi kikazi.
‘Akianika mwanya’ katika mazungumzo
na Amani juzikati, Johari alisema haoni sababu ya kuficha ukweli kuwa
bila Ray isingekuwa rahisi yeye kufika alipo kisanii hivyo lazima
akumbuke kurudisha shukrani.
Comments
Post a Comment