TUZO ZA FILAMU 2015 ZAFANA, SERIKALI YAHAIDI NEEMA
Mama yake na Steven Kanumba akipokea tuzo ya mchango mkubwa kwenye
filamu aliyotwaa mwanaye (marehemu Kanumba) kwenye tuzo za Filamu 2015.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenela Mukangala akitoa shukrani baada ya kupokea tuzo
aliyopewa Rais Jakaya Kikwete na Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA)
kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015.
Mama yake na Steven Kanumba akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo
ya mwanaye kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana. Mama yake na Steven Kanumba akilia baada ya kuitwa ampokelee tuzo mwanaye. Irene Paul (Best Actress) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.
Irene Paul (Best Actress) akipongezwa na Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala kwenye hafla ya Tuzo za
Filamu 2015 jana.
John Kalage (Best Director) akipokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.
Hissan Muya (Best Actor Supporting Role) akipeana mkono na viongozi wa
meza kuu wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo yake kwenye hafla ya
Tuzo za Filamu 2015 jana.
Grace Mapunda (Best Actress Supporting Role) akipeana mkono na Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada
ya kupokea tuzo yake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.
Hissan Muya (Best Actor Supporting Role) akipokea tuzo kwa niaba ya msanii mwenzake kwenye hafla ya Tuzo za Filamu 2015 jana.
Mwakilishi wa Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian Tanzania Film
Awards 2015) akipeana mkono na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenela Mukangala mara baada ya kupokea tuzo kwenye Tuzo za
Filamu 2015 jana.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala
pamoja na viongozi mbalimbali wa meza kuu kwenye hafla ya Tuzo za Filamu
2015 wakipiga picha na baadhi ya washindi wa Tuzo za Filamu 2015 jana
zilizofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
SERIKALI imesema itaendelea kuweka mfumo mzuri na
kujenga mazingira mazuri ili kuhakikisha biashara ya filamu inaimarika,
ikiwa ni pamoja na kuwavutia wawekezaji binafsi waliopo tayari kuwekeza
katika tasnia ya filamu.Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi wa Tuzo za Filamu 2015, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala alipokuwa akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo za filamu.
Dk. Mukangala alipongeza juhudi za baadhi ya wafanyabiashara wa filamu na wasambazaji ya kudhibiti uharamia wa kazi za filamu, lakini aliwataka kuifanya kazi hiyo kwa manufaa ya wadau wote na sio kwa manufaa binafsi.
"...Serikali itaendelea kuhakikisha kwamba mazingira ya kufanya biashara ya filamu yanaimarishwa. Pamoja na hayo ni vyema wasambazaji na wafanya biashara wengine wa filamu wenye uwezo wakaepuka kulidhibiti soko la filamu kwa nanufaa yao binafsi ili kujenga ushindani sawa," alisema Dk. Mukangala.
Aliwataka wasanii na wadau wote wa filamu kuhakikisha wanaboresha kazi zao zaidi na kufuata vigezo vinavyotambulika ili kuzitangaza kazi zao hata nje ya nchi. "Napenda mtambue kuwa ubora wa bidhaa za filamu ni moja ya vigezo vya kuwa na soko bora la filamu, kwani filamu bora hujitangaza zenyewe. Tuhakikishe kuwa tunaongeza weledi na ubunifu. Hivi ndivyo vigezo vilivyoifanya sekta ya filamu nchi zilizoendelea kufika hapo ilipo," aslisema Waziri Dk. Mukangala.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA), Simon Mwakifwamba aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kujenga chuo maalumu kwa ajili ya filamu ili kuijengea uwezo zaidi tasnia kwani inamchango mkubwa katika kuzalisha nafasi za ajira kwa makundi anuai.
Waliojishindia tuzo za filamu kwa mwaka huu 'Tanzania Film Awards 2015 (TAFA)' katika vipengele mbalimbali ni pamoja na Irine Sanga (Best Screen Play), Hissan Muya (Best Actor Supporting Role), Grace Mapunda Best Actress Supporting Role), Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian), Irene Paul (Best Actress), John Kalage (Best Director) na wengineo.a
Tuzo za filamu nchini ‘Tanzania Film Awards’ 2015 (TAFA). Tuzo hizi kubwa ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere International Conference Center. Zimewezeshwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, TRA, EATV na EAR, International Eye Hospital, Foreplan Clinic, R&R Associates, Simu Tv na Barazani Production.
Comments
Post a Comment