KIONGOZI WA CHAMA CHA UPINZANI BURUNDI AUAWA
KIONGOZI wa chama kidogo cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi katika Mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura.
Mwili
wa Zedi Feruzi amabye alikuwa kiongozi wa Chama cha Union for Peace and
Development ulipatikana nje ya nyumba yake kwenye mji wa Bujumbura.
Juzi
Ijumaa watu wawili waliuawa katika maandamano hayo yaliyochukua wiki
kadhaa huku watu zaidi ya 100,000 wakiwa wameihama nchi hiyo kutokana na
vurugu hizo za kupinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais
kwa muhula wa tatu.
Comments
Post a Comment