SALMA DAKOTA WA ITV AVISHWA PETE, APOTEZA FAHAMU!
Mtangazaji wa ITV na redio, Salma Dakota hivi karibuni alipoteza fahamu baada ya kufanyiwa ‘sapraizi’ ya kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, Gharibu DumbaTukio hilo lilitokea kwenye Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo alikwenda bila kujua kuwa mtu wake huyo alikuwa na jambo kubwa la kumfanyia. Ilielezwa kuwa, Salma akiwa hana hili wala lile, alishangaa akivishwa pete ya dhahabu yenye kito cha Tanzanite ambayo gharama yake ni takriban shilingi milioni 3.
Comments
Post a Comment