Mh.Mbatia: Jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake
Serikali imeshauriwa jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake ambao kwa sasa unalalamikiwa kwa sehemu kubwa na wananchi kwa kukiuka haki za binadamu.
Akizungumza jana mjini Dodoma katika kuhitimisha hoja kuhusu
kukamatwa kwa kiongozi wa wa chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba na
wanachama wake,Mbatia alisema kuwa kitendo hicho kilikiuka haki za binadamu
ikiwemo wanawake kudhalilishwa kijinsia.
Mh. Mbatia emeongeza kuwa ili chaguzi zijazo ziwe za amani na utulivu
ameishauri serikali kubadilisha sera za vyama vya siasa na utawala
pamoja na mfumo wa jeshi la polisi kuendeleza amani na utulivu ambavyo
kwa sasa vinaonekana kuanza kutoweka.
Comments
Post a Comment