Baada ya kufikisha miaka 40 na hakuna aliye jitokeza hata kumchumbia, aamua kujioa mwenyewe
Yasmin Eleby hakupata mchumba wa kumuoa mtu ambaye alitaka awe mume
wake atakapofikisha miaka 40--kwa hivyo akafanya kitendo ambacho
kimewashangaza wengi, aliamua kujioa mwenyewe.
Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby
aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza
miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili
kusherehekea miaka yake 40.
Duru zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake mwenyewe
katika makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na
wageni wengine waalikwa.
Kwa sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio, kwani ni
kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati ya
watu wawili.
Kulingana na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo, sherehe hiyo
ilionekana kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani
makavazi hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi
zao hapo.
Aliposikia
kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini alikuwa anapanga
kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea mwenyewe.
"Eleby alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi na mtu
mwenye nia ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr
ambaye anasema harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika
mitandao ya kijamii.
Anasema
anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba mtu anaweza
kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu
kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.
"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.
Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia
mwenyewe, huenda akapata ushindani. "ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii
na anasifika duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi.
Comments
Post a Comment