UBOVU WA MELI YA MV VICTORIA WAZUA MAKUBWA, ABIRIA WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA MKOA
Meli ya MV Victoria inayofanya safari zake kutoka mkoani Kagera kuelekea jijini mwanza imezuiliwa kuondoka mjini bukoba kutokana ubovu ilionao hali ambayo imewalazimu wananchi waliokuwa wanataka kusafiri na meli hiyo kuandamana hadi kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera kwa ajili ya kutoa malalamiko yao.
Wakiongea nnje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela wananchi hao wamelalamikia kuto kuwepo kwa usafiri wa meli kwa zaidi ya mwezi moja sasa na kwamba jana meli hiyo imewasili mjini Bukoba na kuambiwa wapakie mizigo yao ndani ya meli hiyo kwaajili ya kuisafirisha kutoka mkoani kagera kueelekea jijini Mwanza ambapo wamesema wamepakia mizigo yao ndani ya meli hiyo na leo wameambiwa meli hiyo haitosafiri kutokana na meli hiyo kuwa na hitilafu tangu muda mrefu na kwamba mazao yao biashara sasa yamekuwa yakiharibika ndani ya meli hiyo hali Ambayo imewalazimu wananchi hao kuandamana mpaka kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa kagera kwaajili ya kutoa malalamiko yao juu ya meli hiyo.
Akizungumza na wananchi hao mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi.Sipora Pangani amewataka wananchi hao kuwa na subira na kuwataka waondoke katika ofisi hizo huku akisema kuwa serikali italishughulikia suala hilo huku mbunge wa viti maalum Conchesta Rwamulaza akiitaka serikali kuiondoa meli hiyo kwakuwa imekuwa ikileta hofu kubwa kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake meneja wa SUMATRA mkoa wa Kagera Alex Katama amesema meli hiyo ilisimamishwa kufanya kazi tangu ilipo pata hitilafu kwa ajili ya matengenezo lakini juzi meli hiyo iliondoka jijini Mwanza hadi mjini Bukoba bila Ruhusa kutoka kwenye mamlaka husika na akaongeza kuwa meli hiyo sasa ni mbovu na haifai kutoa huduma yoyote mpaka itakapo fanyiwa marekebisho.
Comments
Post a Comment