MFANYAKAZI WA NDANI ALIYEMTESA MTOTO NCHINI UGANDA ATUPWA JELA MIAKA 4
Jolly Tumuhirwe apatikana na hatia ya kumtesa mtoto mdogo na kufungwa jela miaka 4
Yaya wa Uganda aliyejipata pabaya kwa kumchapa mtoto wa mwajiri wake, amehukumiwa jela miaka minne kwa kosa la kumtesa mtoto.
Kisa cha
yaya huyu kilizua hasira miongoni mwa watu wengi katika mitandano ya
kijamii pale kanda ya video iliibuka mitandaoni ikimwonyesha yaya huyo
akimchapa na kumkanyaga mtoto mwenye mwaka mmoja unusu.
na kumkanyaga mtoto huyo pamoja na kumzaba kofi.
Mnamo
siku ya Ijumaa, Jolly alikiri kumshambuilia mtoto akisema alikuwa
analipiza kisasi kwani mamake mtoto huyo naye alikuwa amezoea kumchapa.
Hata
hivyo mama huyo alikanusha madai ya Jolly ambaye polisi walikuwa
wamesema wangemshitaki kwa kosa la jaribio la mauaji ila kiongozi wa
mashitaka akasisitiza kuwa ingekuwa vigumu kuthibitisha hilo.
Hakimu mkuu Lillian Buchan aliambia Tumuhirwe kwamba alitenda uhalifu ambao hauna hata kisingizio.
Alisema adhabu aliyompa inamtosha kulingana na makosa yake kwa kumtesa mtoto ambaye hana hatia.
Babake mtoto huyo, Eric Kamanzi alisema aliweka kamera ya siri nyumbani kwake baada ya kuwa na shauku kumhusu mfanyakazi huyo.
Kanda ya
video iliyomuonyesha Jolly akimtendea unyama mtoto, ilitoka kwenye
kamera ambayo Bwana Kimanzi aliweka nyumbani kwake baada ya kushuku kuwa
mtoto wake alikuwa anatendewa unyama na pia baada ya kumapata mtoto
wake akiwa na alama za majeruhi mwilini mwake.
Alimshitaki mwanamke huyo kwa polisi na kisha kuisambaza kanda hio kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya hukumu kutolewa,Kamanzi alisema: "sio juu yetu kuamua adhabu anayofaa kupewa Jolly. ''
"tunatumai
kuwa hili ni funzo kwa wafanyakazi wengi wa nyumbani kwamba huwezi tu
kwenda kwa nyumba ya mtu na kumtesa mtoto na kutarajia kuondoka tu kama
ulivyoingia. ''
Comments
Post a Comment