AIBU:WABONGO WAFUMANIANA CHINA....WAZICHAPA KAVUKAVU,WAVUANA NGUO BARABARANI NI NDANI YA SWAUM KALI

Ni aibu kubwa kwa taifa! Huku Waislamu wakiendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, warembo wawili, raia wa Tanzania (Wabongo), mmoja mkazi wa Sinza, Dar aliyetajwa kwa jina moja la Glory na mwingine ambaye jina halikupatikana,
wanadaiwa kufumaniana laivu nchini China na kugeuka kituko cha aina yake, Ijumaa Wikienda ndilo lenye uthubutu wa kuripoti tukio hilo.




Warembo wawili, raia wa Tanzania (Wabongo), mmoja akifahamika kwa jina moja la Glory na mwingine ambaye jina halikupatikana wakikwidana.
Habari za awali zilidai kuwa Glory ndiye aliyemfuma mwenzake na bwana’ke, raia wa Nigeria kisha kumshushia kipigo kabla ya kutoana nje na kwenda kuchaniana nguo barabarani, mchana kweupe.
OFM KUTOKA GUANGZHOU, CHINA
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu, mwakilishi wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers nchini China (jina kapuni), alisema kuwa akiwa katika pitapita zake za kukusanya matukio ili kuyatuma Bongo kuonesha jinsi gani Wabongo wanavyoidhalilisha nchi yao ughaibuni, wikiendi iliyopita alitembelea eneo la Guangzhou Rujing Lu Sky Coffee nchini humo ambalo Watanzania wengi hufanyia ‘biashara’ zao.


Raia hao wakizichapa kwa ghadhabu.
Mwakilishi huyo wa OFM alisema akiwa eneo hilo linalosifika kwa matukio na starehe za kichumbani ndipo alipokumbana na timbwili hilo ambalo linaichafua taswira ya Wabongo ambao wanakwenda China kuchukua biashara mbalimbali.
NI AIBU KUBWA
“Dah! Hii ni aibu kubwa ambayo sijawahi kutegemea kuwa nitakutana nayo, yaani Wabongo kwa Wabongo wanapigana, wanachaniana nguo na kuumizana kisa bwana wa Kinigeria, tena ughaibuni!” Alisema kwa masikitiko mwakilishi huyo wa OFM nchini China.


Raia wa kichina wakishuhudia live vimbwanga hivyo.
Akiendelea kufunguka, OFM alisema kwamba ilisemekana kuwa Mnigeria huyo aliwahi kuwa na uhusiano na Glory hivyo siku ya tukio, jamaa alimtosa Glory na ‘kuchepuka’ na mwenziye.
KIPIGO CHA MBWA MWIZI
Ilielezwa kwamba Glory hakukubali ndipo akamuanzishia timbwili mwezake na kumpa kipigo cha mbwa mwizi akimtuhumu kwa nini amemchukulia bwana’ke.
WASABABISHA FOLENI
Katika timbwili hilo, warembo hao walijikuta wakichaniana nguo na kubaki nusu utupu huku wakirushiana matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini kimaadili).
Wakati wakipigana waliingia barabarani na kusababisha bonge la foleni huku wakinusurika kukanyagwa na magari hasa walipoangushana katikati ya barabara.


Kachero wa kichina akiamulizia ugomvi huo.
POLISI WAITWA
Kuna wakati Glory alimkaba mwenzake hadi mashuhuda wa sinema hiyo ya bure wakahisi anamuua mwenzake hivyo kulazimika kuita polisi wa usalama barabarani ambaye alifika mara moja na kuwaamulia.
Ilisemekana kwamba, askari huyo alipoona hawaelewani lugha ndipo akawaachia huku kila mmoja akichukua hamsini zake.
GLORY ANASEMAJE?
Baada ya kupata taarifa hizo, Ijumaa Wikienda lilifanya jitihada za kumtafuta Glory kwa njia ya simu yake ya kiganjani lakini hakupokea na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kuhusiana na tukio hilo, licha ya kuonekana umemfikia (delivered) hakujibu hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.

Mmoja kati ya warembo hao waliokuwa wakizichapa.
YATOKANAYO
Kumekuwa na wimbi la warembo ambao huenda nchini China kwa kisingizio cha kwenda kuchukua biashara lakini ukweli ni kwamba huenda kufanya mambo mengine mabaya (hasa biashara haramu ya kuuza miili).
Mbali na ukahaba, wapo wanaodaiwa kufanywa punda wa kubeba madawa ya kulevya na matokeo yake ni kuishia kunyongwa mara wanapokamatwa.
Hata hivyo, baadhi ya Wabongo waliozungumza na gazeti hili kutoka China, waliziomba mamlaka husika kushughulikia suala hilo hasa wanapotoa vibali vya kutoka nje ya nchi wajue mhusika anakwenda kufanya nini.

Comments

Popular posts from this blog