WATANZANIA 65 KUNYONGWA CHINA KWASABABU YA MADAWA YA KULEVYA

Vijana 65 wa Tanzania wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya. 
Vijana hao ni kati ya zaidi ya 403 wa Tanzania wanaoshikiliwa katika nchi mbalimbali duniani kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara hizo. 
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, mjini Dodoma wakati akizungumzia Maadhimisho ya Siku Dawa za Kulevya Duniani yanayofanyika Juni 26 kila mwaka. 
Lukuvi alisema kuwa kwa mwaka huu maadhimisho hayo ya kesho, kitaifa yatafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nzovwe jijini Mbeya na Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
 Tangu mwaka 2008 kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wenye asili ya Kitanzania kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi, mpaka hivi sasa idadi yao ni kubwa kiasi cha kufikia zaidi ya 400, na wanashikiliwa katika nchi mbalimbali ambazo pia adhabu zao zinatofautiana kulingana na sheria za nchi hizo
alisema Lukuvi.

Comments

Popular posts from this blog