SOMA ALICHOSEMA BUNGENI MBUNGE WA ARUSHA GODBLESS LEMA NA KUZUA KIZAAZAA
Mbunge
wa Arusha mjini Godbless Lema ni miongoni mwa waliowasha vipaza sauti
kwenye bunge la bajeti linaloendelea Dodoma ambapo sehemu ya
alichochangia ni hiki kinachofata hapa chini.
‘Dola
bilioni moja miaka kumi nyuma ilikua ni Trilioni 11 lakini sasa
unaongelea Trilioni 17 kwa hiyo shilingi imeshuka thamani lakini
unashangaa kwanini tunaendelea kuongeza ushuru kwenye pombe na sigara
kama chanzo cha mapato ya taifa letu, nchi nyingi duniani zinazoongeza
ushuru kwenye pombe na sigara lengo lake ni kuona idadi ya wanaokunywa
na kuvuta inapungua tofauti na Tanzania ambako lengo limekua ni
kukusanya mapato, hiki ni kitu cha kusikitisha sana’
‘Nimekwenda
Singida hivi karibuni kwenye ziara ya chama chetu na Mh. Tundu Lissu,
ukiwa Singida na Dodoma unaona kuna jua kali… Singida Same serikali
imeweka vikao barabarani >> NENDA POLEPOLE HAPA KUNA UPEPO MKALI
UNAUA << ingekua ni taifa kama Israel, upepo mkali hauwekewi vibao
vya kuua bali upepo mkali unachukuliwa kuwa umeme’
‘Sehemu
kubwa ya Singida na Dodoma ni semi desert, serikali ingeweza
kabisakabisa kutengeneza solar village maeneo haya ikatengeneza umeme
mkubwa kupitia nguvu za jua ukaingiza kwenye gridi ya taifa na mngeweza
kupunguza bili za umeme ambazo Wananchi kwa sasa wanapigwa huko mitaani’
‘Hata
kama kutakua na mpango wa aina gani, unapokua na serikali ambayo
haifikirii kwa upana… serikali ambayo inasema bado inakopesheka, bado
tunaweza kukopesheka…. mimi ningekua ni nyinyi, ningekwenda kukopa
barabara zote nchi nzima zijengwe, ningeenda kukopa reli ijengwe,
ningekwenda kukopa Airport ziboreshwe na ningekwenda kukopa serikali
yenu ihamie hapa Dodoma’
‘Watu
wengi wamesema kuhusu serikali kuhamia hapa Dodoma, ukiondoa serikali
Dar es salaam ukaileta Dodoma utaipa nguvu hii Ruaha ambayo hakuna
watalii, watalii wataanza kwenda kwa sababu wakuu wote wa nchi watakuwa
wanakuja Dodoma kufanya mikakati yao kwa hiyo centre ya mapumziko itakua
ni Iringa, Mbeya na Singida hapa’
‘Mimi
ningekua nyinyi ningefanya maamuzi magumu, ningechukua Mawaziri wote na
makatibu wakuu wote waje hapa wakae gesti na wengine wakae kwenye
matent kwa sababu msipochukua maamuzi serious hamuwezi kuibadili hii
nchi, hii nchi haitobadilishwa kwa Kinana kuzunguka kutafuta kura za
Urais huko kote anakokwenda’
Comments
Post a Comment