Putin akutana na rais wa Ukraine



Putin akutana na rais wa Ukraine Petro Poroshenko
Marais wa Urusi na Ukraine wameongea kwa mara ya kwanza.
Vladmir Putin na Rais aliyechaguliwa nchini Ukraine, Petro Poroshenko, walikutana kwa muda mfupi kabla ya chakula cha mchana katika maadhimisho ya miaka 70 tangu mataifa ya Ulaya kukombolewa kutoka kwa Wanazzi.
Maafisa wa Serikali wa Ufaransa walisema kuwa katika mashauriano ya viongozi hao wawili ambayo hayakuwa rasmi yaliyoandaliwa na Rais Fransois Hallande, Bwana Putin na Bwana Poroshenko walikuwa wamekubali kuwa mashauriano juu ya kusitisha mapigano katika Ukraine Mashariki yatafanywa hivi karibuni.Maadhimisho hayo yanaendelea nchini Ufaransa.

Maafisa hao walieleza kuwa viongozi hao wawili walizungumza juu ya kuzorota kwa uchumi kunakotokana na ghasia za kisiasa nchini Ukraine.
Baadaye Kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel, amehimiza Urusi kutekeleza wajibu wake kupunguza uhasama unaoendelea kupanda nchini Ukraine.

Comments

Popular posts from this blog