JOSHUA NASSARI (MB) KUFANYA HARUSI YA ALAIKI KESHO JIMBONI KWAKE
Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Meru Dr Paul Akyoo akifanya maombi kwa Bw Joshua Nassari ,Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki na Bi Anande Nnko wanaotarajia kufunga ndoa Jumamosi hii. |
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru. |
Bi ,Harusi Mtarajiwa Anande Nnko akimpatia zawadi ya T-Shirt Mumewe Mtarajiwa Bw Joshua Nassari wakati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwao Meru. |
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.
Kwa
Mujibu wa Mh Nassari ,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba
mchana watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi
jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna kadi.
"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!"alisema Nassari.
Na
ssari amesema watu zaidi ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe
hiyo ya aina yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo
mbalimbali .
Na Michuzi Media Group
Na Michuzi Media Group
Comments
Post a Comment