HIZI NI SABABU ZA WANAUME KUOTA MATITI



Kitaalamu, tatizo hilo hujulikana kama,gynecomastia nalo ni kukua kuliko kawaida
kwa tishu ya kwenye titi inayojulikana kamaglandular tissue.

Ni nadra kujitokeza, lakini kwa siku zakaribuni baadhi ya wanaume wana
maziwa kama walivyo wanawakeTatizo la kuota matiti kwa wanaume na
watoto wa kiume limekuwa kubwa katikadunia ya leo.

Inawezekana wakati unatembea njianiukaona wanaume au watoto wadogo wa
kiume wakiwa na matiti tena makubwaambapo watu wengi  huchukulia kama ni
kawaida. Kitaalamu, tatizo hilo hujulikanakama, gynecomastia nalo ni kukua kuliko
kawaida kwa tishu ya kwenye titiinayojulikana kama glandular tissue.
Tatizo hili huonekana zaidi kwa watotowachanga na  wanaume walio katika umri
wa kubalehe, lakini pia huonekana kwawatu wazima na wazee.

Ukubwa wa tatizoAsilimia 60-90 ya watoto wachanga
wanapata tatizo hili la kukua kwa matiti kwampito linalojulikana kitaalamu kama,
transient gynecomastia kutokana nakuwepo kwa kichocheo cha aina ya
estrogen kwa wingi wakati wa ujauzito wamama.Kati ya asilimia 4-69 ya vijana walio katika
umri wa kubalehe  imeonekana wanapatatatizo hili kutokana na  kuwepo kwa wingi
kwa kimeng'enyo aina ya estradiol. Maranyingi huonekana katika umri kati ya miaka
10-12 na hupotea taratibu ndani ya miezi18, si kawaida yake kuonekana kwa vijana
walio na umri wa zaidi ya miaka 17.

Asilimia 24-65 ya watu wazima hupatwa natatizo hili, hii hutokana na kubadilishwa
kwa wingi kwa kichocheo aina yatestosterone kuwa estradiol na kutolewa
kwa uchache kwa kichocheo hiki chatestosteron kutoka kwenye korodani
ziazoanza kuzeeka..Ikumbukwe ya kwambakichocheo hiki testosteron hutengenezwa
katika korodani. Kichochezi cha testosteronndicho kichochezi kikuu cha kiume
kinachowezesha tabia za kimwili za kiume.

Nini hutokea?
Kuongezeka ukubwa wa matiti kwawanaume hutokana na kuharibika kwa
mfumo wa vichocheo unaojulikanakitaalamu kama, estrogen-androgen balance
na hivyo kusababisha estrogen kutolewakwa wingi ama kuongezeka kwa msisimko
wa matiti kwa kiwango cha zaidi yakawaida kwa kichocheo aina ya estrogen
kilicho kwenye mzunguko wa damu.
Kichocheo hiki husababisha chembechembe
zinazojulikana kama ductal epitheliakuongezeka kwa wingi, kurefuka na
kugawanyika, kuongezeka kwachembechembe za mafuta na kuongezeka
kwa mfumo wa damu kwenye matitihutengenezwa kutoka kwenye vichocheo
vya testosteron na androgen kwa kutumiakimeng'enyo kinachojulikana kama
aromatase.

Aina za tatizo hili
-Puffy nipples -Kuongezeka ukubwa wachuchu za matiti kutokana na kuongezeka
kwa tishu aina ya glandular.
-Pure glandular gynecomastia - Huonekanazaidi kwa wale wanaofanya mazoezi ya
kujenga mwili, kutokana na matumizi yadawa za kujenga mwili ambazo zinakuwa
na kiwango kikubwa cha kichocheo aina yatesterone, ambacho hubadilishwa kuwa
estrogen.

Kwa wanaume wembamba, tatizo hili
hutokea kutokana na kuongezeka kwa tishu
za tezi za maziwa (breast tissue gland)
pamoja na kuwepo/kutokuwepo kwa tishu
aina ya adipose.

Ni nani aliyeko  hatarini?
1.Wanaume walio na umri zaidi ya miaka 50. 


2.-Wenye uzito uliopitiliza
 

3.Unywaji pombe kupindukia
 

4.Magonjwa sugu ya figo au ya ini
 

5.Kuwepo kwa historia ya tatizo hili katika
familia.
Visababishi vya kukua kwa matiti kwa
wanaume

-Pseudogynecomastia - Kuongezeka kwatishu zinazozunguka chuchu za matiti na
huambatana na kuwepo kwa wingi watishu aina ya adipose. Mazoezi na kula
vyakula venye virutubisho sahihi huondosha tatizo hili.

-Unilateral/asymetrical gynecomastia - Ni kuongezeka kwa titi moja pekee au la
upande mmoja wa mwili wa mwanamume kutokana na sababu mbalimbali. Titi la
upande wa pili huwa kwenye umbile na saizi ya kawaida. Bilateral gynecomastia ni
kuongezeka kwa matiti yote mawili.

-Hypogonadism - Kutofanya kazi kwa korodani vizuri  na kuwa ndogo. Hii
husababishwa na magonjwa mbalimbali.

-Umri - Kuzeeka pia kumehusishwa kutokea kwa tatizo hili kutokana na kutolewa kwa
uchache   kwa kichocheo cha testerone na kuongezeka kwa juhudi za kutengeneza
kwa wingi kwa kimeng'enyo aina ya estradiol kutoka kwenye kichocheo aina ya
testerone
.

Pia, mabadiliko ya mfumo mzima wa
vichocheo mwilini hasa kwa wale wenye
uzito uliopitiliza.

-Uzito uliopitiliza
- Watu wenye uzitouliopitiliza hupatwa na tatizo hili kutokana
na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo mwilini na hivyo kuongezeka kwa
kichocheo aina ya estrogen mwilini mwao na wakati huohuo kupungua kwa
kichocheo kingine aina ya testerone.

-Saratani - Baadhi ya saratani kama vile ya kwenye korodani, tezi lililo juu ya figo,
saratani ya tezi la kichwa, huharibu mfumo mzima wa vichocheo mwilini hasa wa
kuweka sawa vichocheo kati ya uanaume na uanawake (male-female hormonal balance).

-Hyperthyroidism - Kukua kwa ukubwa wa tezi la koo na hivyo kutengeneza kwa wingi
kichocheo aina ya thyroxine.

- Tatizo la figo kushindwa kufanya kazi -Nusu ya wagonjwa wote wanaotibiwa
tatizo la figo kushindwa kufanya kazi kwa kutumia hemodialysis hupatwa na tatizo hili
la kukuwa kwa matiti kutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo
mwilini.

-Matatizo ya Ini -  Dawa za kutibu magonjwa ya kwenye Ini kama kuoza kwa
ini, ini kushindwa kufanya kazi husababisha kutokea kwa tatizo hili kutokana na
kukosekana kwa uwiano sawa wa mfumo wa vichocheo mwilini.

-Utapiamlo, ukame - Utapiamlo, ukame au kujikondesha husababisha kupungua kwa
kichocheo aina ya testerone na kuongezeka kwa kichocheo aina ya estrogen na hivyo
kuharibu mfumo wa vichocheo mwilini. Hii hutokana na kukosekana kwa
virutubisho sahihi mwilini ambavyo vingi husaidia kurekebisha mfumo wa vichocheo
mwilini na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa  mbalimbali pamoja na tatizo hili.

-Madhara ya dawa za kurefusha maisha(ARVs)
kwa wagonjwa wa Ukimwi.


-Utumiaji wa  dawa za kulevya kama bangi/ marijuana.

Comments

Popular posts from this blog