ABIRIA AFIA NDANI YA BASI MKOANI KILIMANJARO

WATU wawili wamefariki dunia mkoani Kilimanjaro katika matukio tofauti, likiwemo la mmoja aliyekutwa amekufa akiwa katika basi la Kampuni ya Kilenga akiwa safarini kuelekea mkoani Arusha.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Moita Koka, alisema kuwa mtu huyo ametambuliwa kwa jina la Sayuni Joel (53), mfanyabiashara, mkazi wa Mwembe, wilayani Same, Kilimanjaro.
Akizungumzia mazingira ya tukio hilo, Kamanda Koka alisema Joel alipanda basi hilo T 398 BAT na kwamba kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa akisumbuliwa na tumbo na alikuwa akielekea hospitali kupata matibabu.

Alisema Joel aligundulika kuwa amepoteza maisha baada ya gari hilo kuingia katika stendi kuu ya mabasi Moshi.

Maiti yake imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC huku uchunguzi wa chanzo cha kifo hicho ukiendelea.

Katika tukio jingine, mkazi wa Kijiji cha Kilema – Kiyou, Kata ya Kilema, wilayani Moshi, Martin Michael (45), amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema lilitokea juzi, saa 8 mchana na kudai kwamba amefikia uamuzi huo kutokana na kuchoshwa na hali yake kiafya ambayo imemfanya kutumia dawa kila mara na kwamba kabla ya tukio hilo aliwahi kusikika akilalamikia hali hiyo.

Na Dixon Busagaga, moshi

Comments

Popular posts from this blog