WATU WANNE WAUAWA, 9 WALAZWA KWA MAPIGANO IGUNGA...

Mmoja wa majeruhi wa mapigano hayo akiwa amelazwa hospitalini.
Watu wanne wamekufa na  wengine tisa  wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya hiyo mkoani Tabora, kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji, yaliyotokea  katika Kijiji cha Isakamaliwa wilayani Igunga. 
Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Elibarik Kingu alitaja waliofariki ni Chawala Doke, Mohammed Msengi, Biblo Kingu na Peter Karongo, wote wakazi wa Kijiji cha Isakamaliwa.
Mapigano hayo yalitokea juzi saa 7 mchana. Kingu alisema pia nyumba 12 zimechomwa moto na uharibifu mkubwa wa mali za wakazi wa kijiji hicho.
Wafugaji wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, pembezoni mwa mto Manonga, ndiyo wanatuhumiwa kufanya mauaji. 
Kwa mujibu wake, zaidi ya watu 20 hawajulikani waliko  na zaidi ya watu 150 hawana makazi, kutokana na nyumba zao kuchomwa moto kwenye mapigano hayo. 
Chanzo cha mapigano ni wafugaji kulisha mifugo katika mashamba ya wakulima wilayani Igunga. 
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora na ya Mkoa wa Shinyanga, zilifika eneo la tukio na kushuhudia uharibifu uliofanyika.  Kikao hicho kiliendelea kupata usuluhishi wa mgogoro huo  na kuchukua hatua kwa waliohusika katika mauaji na uharibifu.CHANZO NA ZIRRO BLOG

Comments

Popular posts from this blog