WATOTO WAWILI WA FAMILIA MOJA WATEKETEA KWA MOTO.....





Watoto wawili wa kiume wa familia moja, Daniel Paul (8) na mdogo wake, Emmanuel Paul (3), wamepoteza maisha wakiwa pamoja baada ya kuteketea kwa moto ndani ya nyumba.
Tukio  hilo lilijiri majira ya saa 1:00 asubuhi, maeneo ya Mtaa wa Rufita, Mwanza-Road mjini Tabora  baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani.
Habari za awali zilieleza kuwa chanzo cha moto huo kilidaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme na kuisababishia familia hiyo majonzi makubwa ya misiba miwili kwa mpigo.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora,  OCD, Samwel Mwampashe alithitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kuwa polisi watafanya uchunguzi ili kubaini chanzo kamili cha moto huo

Comments

Popular posts from this blog