MWALIMU AMVUNJA MGUU MWANAFUNZI KISA MAPENZI
Mwalimu huyo alifikia hatua ya kumfuata nyumbani kwao machi,22,2014 saa 12.30 jioni hali iliyowashtua wazazi na kumuhoji mtoto juu ya hilo ndipo binti alipokwenda shule Machi,24,2014 alimuliza mwalimu huyo sababu ya kumfuta kwao, hali hiyo ilimchefua mwalimu na kutoa maneno ya kashfa na kumpiga vibao vya uso na kusababisha maumivu mbalimbali ya mwili wake ikiwemo kuvunjika kwa mguu.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Maweni Macris Yakayeshi akiri mwanafunzi huyo kuvunjika mguu wa kulia sambamba na kuvimba uso na kupelekea mdomo kwenda upande na wiki ijayo anatarajia kumwekea `P.O.P’.
Dr.Yakayeshi alibainisha kuwa kutokana na tatizo alilonalo itamlazimu kukaa na mhogo si chini ya wiki sita ili mguu utengamae sambamba na kuitaka jamii ibadilike na matukio ya udhalilishaji wa kijijnsia huku akidai alifikishwa hapo kifua kikiwa wazi ili hali binti ni rika la balehe na kuomba sheria ichukue mkondo wake.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kamala katani humo Curthbert Kusongwa alisema, kwa maelezo aliyoyapata kutoka kwa walimu wa shule hiyo walidai binti alikataa adhabu aliyopewa na kumpiga kofi mwalimu na ndipo mwalimu akamwambia akamlete mzazi wake,wazazi walipofika alidai alimvamia mwalimu na kuanza kumpiga hali iliyolazimu jeshi la polisi kuingilia hekaheka kiyo.
Akizungumzia tukio hilo Athumani Moshi ambaye ni baba wa Zubeda alisema alishangaa kumuona mwanae amerudishwa shule huku akiwa amevimba uso na mdomo ndipo akadai kuitwa na mwalimu husika,alipofika shule na kuonana na mwalimu husika hakuwa muungwana kutokana na kauli chafu na kebehi.
Moshi alisema baada ya kauli hizo ghafla mwalimu akamkata mtama mwanae na kuanguka chini ndipo wakapigana,huku akikiri awali alipata kuelezwa juu ya adha ya mwalimu huyo kwa binti yake hadi kufikia hatua ya kumfuata usiku siku za mapumziko sanjari na kumpa adhabu zisizostahili kwa kisa alikataa kuwa nae kimapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa Zedekia Makunja alipoulizwa kama analifahamu hili akadai naam ila wataitwa machi,31,mwaka huu.
Kwa nyakati tofauti Mariamu Issa na Winyfrida Bwire walisema sheria ya mwanafunzi juu ya adhabu inajulikana ,walimu hawana budi kulea watoto kwa kuwafundisha adabu ,huku wakidai kuna namna kati ya mwanafunzi na mwalimu haiwezekani kukataa kwa adhabu amvunje mguu.
Comments
Post a Comment