APONDWA MAWE NA KUCHOMWA MOTO BAADA YA KUKUTWA NA PIKIPIKI YA WIZI..

Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-30 ameuawa kikatili kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na wananchi waliojichukulia sheria mkononi baada ya kukamatwa na pikipiki ya wizi Katika kijiji cha Kagongwa Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa nane mchana mara baada ya marehemu kuiba Pikipiki hiyo yenye no T634 CNK Aina ya SanLG mali ya Patrick Seba mkazi wa Nyahanga Mjini Kahama ambayo imeibiwa jana asubuhi Maeneo ya shule ya Kahama Muslim ikiwa imeegeshwa na dereva wake aitwaye Shija Zacharia.

Kwa mujibu wa Mmiliki wa pikipiki hiyo Bwana Seba Ameiambia redio Kahama fm Kuwa alipewa taarifa na dereva wake ambapo aliamua kutoa taarifa ya kupoteza pikipiki hiyo kwa waendesha bodaboda wa mjini Kahama na Kagongwa.Amesema wakati anatoka Kagongwa kutoa taarifa ndipo akakutana na vijana wawili ambao waliokuwa wanaiendesha pikipiki hiyo kuelekea Kagongwa ambapo aliamua kuwafuatilia na kwamba aliwapata katika kijiji hicho.Baada ya kuwasogelea aliizima pikipiki hiyo kwa kutumia remote kwani wakati inaibiwa ilikuwa imezimwa kwa kutumia Remote ambapo walianguka chini na Kuanza kukimbia na wananchi wakaanza kumshambulia mmoja kwa mawe hadi kumuua huku mwingine akifanikiwa kukimbia kusikojulikana.

Jeshi la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwili wa marehemu ulipelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifdadhia maiti kwenye hospitali ya Wilaya ya kahama.

Kwa takribani miezi Miwili na Nusu sasa watu wa wanne wameuawa kwa kuchomwa na moto katika kijiji hicho cha Kagongwa kwa madai kuwa wamechoshwa na kukithiri kwa wimbi la wizi katika Kijiji hicho na maeneo 

Comments

Popular posts from this blog