ANGALIA PICHA ZA WEMA ALIVYOFANYA VURUGU OFISI ZA GLOBAL PUBLISHER
HOVYOOO! Wema Isaac Sepetu aliye pia Miss
Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao
makuu ya Kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar na kuzua
timbwili la aina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na
mpenziwe, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Tukio hilo la kumchoresha staa huyo mwenye
vituko kila kukicha, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global
ambao ni wachapishaji wa gazeti hili (Amani), Uwazi, Ijumaa, Ijumaa
Wikienda, Championi na Risasi majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa
huku wapita njia wakimzodoa kwa maneno ya kejeli.
Wema
akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya 'kuua mtu', mkononi akiwa na
gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto
ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
ATINGA NA WAPAMBE DHAIFU
Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi
wakiongozwa na meneja wake, Martin Kadinda waliosimama nje ya ofisi
hizo, Wema alifika kwa upole akionekana mkarimu kwa mlinzi ambapo
aliomba kuonana na mwandishi nguli wa magazeti pendwa, Imelda Mtema.
Mlinzi alimruhusu kwa vile Global ni
mjengo wa mastaa na watu wasio mastaa, huwa hawakauki kuingia na kutoka
kwa mambo mbalimbali.
Wema alipofika mapokezi, pia aliomba
kuonana na mwandishi huyo lakini tofauti na utaratibu ambapo huwa mgeni
akifika huulizwa kama ana ‘apointimenti’ ili aitiwe anayemhitaji, Wema
alipitiliza kwa nguvu hadi chumba cha habari akifuatana na kijana
aliyekuwa akimrekodi.
Wema akiwa ndani ya News Room akimtafuta mwandishi wa Global Imelda Mtema, huku akisema yeye ni chizi!
Akiwa ndani ya chumba cha habari, Wema aliuliza kwa sauti ya juu na ya kujiamini: “Imelda yupo wapi? Nauliza Imelda yupo wapi?”
WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa
sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba
atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa
maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka
kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
Cha kushangaza, Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kisha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
MSIKIENI WENYEWE
“Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?”
ATULIZWA, AGOMA
Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi
alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema
tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa
na utaratibu.”
Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema
aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu
iliyopita, aliendelea kumng’ang’ania Imelda ambaye alikuwa akijaribu
kumtuliza:
“Wema twende tukakae pale kwenye meza ya
mkutano uwaeleze viongozi wangu tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni
msagaji mbona haipo, ni gazeti gani?”
"Mimi ni chizi, msinitanie ohhh!!
Licha ya kupewa mwongozo huo, Wema aliendelea kufoka:
“Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya machizi wote, ohooo!”
MLINZI ATONYWA, ATIA TIMU
Baada ya hali kuwa tete, mlinzi wa
geti kuu alipigiwa simu ya mezani na kujulishwa juu ya Wema kusababisha
kazi kusimama ambapo alifika haraka tayari kwa kumtoa nje kwa hiyari
yake au lazima.
Ndipo
kukatokea timbwili kubwa, wapambe wake ‘goigoi’ nao waliingia wakitaka
kufanya vurugu ili kumteka mwandishi huyo lakini kikosi imara cha Global
kikiongozwa na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally
kilijiimarisha na kutuliza fujo hizo huku kikiwa makini kuhakikisha Wema
na timu yake hawajeruhiwi hata kidogo.
WEMA ATUMIA GAZETI KAMA SILAHA
Katika purukushani hiyo, Wema alionesha
udhaifu wa kumudu varangati pale alipotumia gazeti aliloshika kumpiga
nalo mwandishi Imelda, jambo lililodhibitiwa kama Waasi wa M23 wa Kongo
walivyodhibitiwa na Majeshi ya Umoja wa Mataifa, akatolewa nje.
Wema akiwa nje ya ofisi sasa baada ya kutolewa kwa nguvu, yeye pamoja na wapambe wake
MBALI NA WEMA
Ukiachia mbali Wema kutulizwa kwa kutolewa
nje kwa nguvu, vijana wake walegevu nao waliwekwa chini ya himaya ya
Global kwa kunyang’anywa kamera ya video iliyokuwa ikitumika kuchukua
matukio huku nao wakipigwa picha za kutosha na wapiga picha wetu.
VITA KUBWA, WEMA AVUA VIATU
Nje ya ofisi, ‘vita’ kubwa kati ya Wema na
walinzi wa Global (alifika mwingine kutoka lindo la mbali) ilizuka
ambapo staa huyo alivua vile viatu vyake virefu vya rangi ya bluu bahari
na kuanza kumpiga navyo mmoja wa walinzi hao akiamini anamkomesha
lakini pia akadhibitiwa!
Wema
akiwa ameshika viatu vyake vya mchuchumio mkononi baada ya kutolewa nje
ya ofisi na wapambe wake akiwemo meneja wake, Martin Kadinda (kulia).
Wema akiwa anarandaranda kwenye geti kuu
akiwa peku, alidondosha matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini
kwa namna yalivyokuwa makali. Ilikuwa si rahisi kuamini kuwa yeye ni
kioo cha jamii.
Timbwili la Wema na wapambe wake akiwemo
Petit Man, ambao hawakufua dafu kwa walinzi na vijana wa Global nje ya
ofisi hizo, lilichukua zaidi ya nusu saa huku likikusanya kadamnasi na
kusababisha mtaa kujifunga wenyewe.
Wema
akiwa kafura ka' faru aliyekoswa koswa kung'olewa kipusa na majangili,
kulia ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
POLISI HAO
Hata hivyo, uongozi wa Global uliwasiliana
na Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao walifika na
kumkuta Wema na timu yake wakiwa wamepoa mlangoni, wakaambiwa timbwili
limetulia hivyo wakatimua zao.
'Baby'
wa Diamond Platnumz alikuwa hashikiki viatu viligeuka kuwa 'mzigo mzito'
akivibagwa chini huku akitoa mkwara akiwa pekupeku na kufunga mta
a.
Ilibidi
askari polisi waitwe kuja kuhakikisha utulivu unakuwepo huku wapita
njia wakiwa hawaamini macho yao kuwa wanayemuona mbele yao 'peku peku'
akimwaga mitusi ni Miss Tanzania, Wema Isaac Sepetu!
APEWA KAMERA, KADI NOOOO!
Baadaye
Wema aliomba kupewa kamera yake ambapo zoezi hilo lilifanyika lakini
‘memori kadi’ yenye picha walizoanza kurekodi, ilitolewa ili kupisha
maridhiano kwanza. Waliambiwa kadi hiyo ilitolewa kwa sababu walirekodi
bila idhini au kibali cha Kampuni ya Global.
Miongoni
mwa watu waliokuwa kwenye msafara wa Wema ni pamoja na Ammy Nando
(kushoto), mshiriki wa Big Brother Africa 'The Chase' ya mwaka jana
ambaye alikuwa akificha sura kukwepa kamera za Global.
WEMA AGOMA KUONDOKA
Baada ya kugundua kadi ya kamera ipo chini
ya ulinzi wa Global, Wema alitaka kulianzisha tena akidai hawezi
kuondoka hadi apewe kadi hiyo lakini uongozi uliweka ngumu. Baadaye
aliondoka kimyakimya. Wakati huo wapambe wake walishaondoka kitambo.
WEMA: CHIZI in action......
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni,
kadi ya kamera hiyo bado ilikuwa inashikiliwa na uongozi wa Global ili
kumthibitishia Wema kuwa hawezi kufanya umafia wowote dhidi ya waandishi
wa kampuni hiyo yenye nguvu kihabari nchini Tanzania
Comments
Post a Comment