WATANZANIA 15 WAHUKUMIWA KUNYONGWA CHINA
Matukio
ya kukamatwa kwa Watanzania nchini China kwa kesi za biashara ya dawa za
kulevya yana idadi kubwa sana ndani ya hii miaka mitano iliyopita.
Miezi
miwili iliyopita Balozi wa Tanzania China alithibitisha kwenye kwamba
Watanzania wasiozidi mia mbili ndio wamefungwa kwenye magereza
mbalimbali ya China kutokana na kesi tofautitofauti ila dawa za kulevya
ndio zinaongoza’
Balozi
huyu alisema kwa wakati huo hakuwa na rekodi yoyote ya Mtanzania
kuhukumiwa kunyongwa au yeyote ambae tayari ameshanyongwa na kwamba kwa
taarifa zaidi Wizara ya mambo ya nje itafutwe.
Baada ya
hayo yote, hatimae katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje John Haule
March 25 2014 ametaja jumla ya Watanzania waliokamatwa kwa kesi ya dawa
za kulevya kwa kusema‘tuna Watanzania wengi tu ambao wapo kwenye
magereza kule China japo tumeshindwa kwa harakaharaka kupata idadi ya
waliojihusisha na shughuli ya dawa za kulevya lakini kuna rekodi fupi
tulizonazo sasa hivi’
Katika
Magereza ya China mpaka February 2014, tumepewa taarifa na Mamlaka za
China kwamba wapo Magerezani Watanzania 177 ambapo 15 kati yao
wamehukumiwa kunyongwa kutokana na biashara hiyo ya dawa akini niseme tu
wenzetu wa Serikali ya China wanatuthamini sana kama sisi
tunavyowathamini’
‘Wenzetu
wa China wanathamini zaidi uhusiano wetu na ndiyo maana hata wale
wachache Watanzania waliohukumiwa kunyongwa hawajanyongwa mpaka leo na
hatutegemei kama watanyongwa, yani sanasana watafungwa kifungo cha
maisha gerezani’.
Comments
Post a Comment