TUNDULISU AZUA BALAA BUNGE LA KATIBA SOMA HAPA

Kikao cha UKAWA ambacho pamoja na mambo mengine Kiongozi wa umoja huo Freeman Mbowe alitoa hoja ya wajumbe wa bunge la katiba kurudi makwao na kuendelea na shughuli nyingine za kuwashawishi watanzania wote huko majimboni wakawahamasishe umma kuikataa katiba ambayo imevamiwa na chama kimoja cha CCM 
Hoja  ambayo iliungwa mkono na idadi kubwa ya wajumbe katika kikao hicho huku wengine wakitaka ile jana wengine wakitaka waondoke leo asubuhi baada ya kushiriki katika session ya asubuhi na baada ya kiapo watu watimke mle ndani lakini baada ya majadiliano mengi na hoja hiyo kuchangiwa lilikuja wazo la Tundulisu ambalo limejigawa katika sehemu tano(5) muhimu ambapo alisema:
(1)Tusivunje bunge kwa hoja dhaifu ila tuvunje bunge kwa hoja nzito hata tukiwaeleza watanzania watufahamu lakini isiwe hatukuchaguliwa katika kamati ya uongozi sababu hiyo tu itufanye tuvunje bunge watanzania watatuona tuna uroho wa madaraka.
(2) Alisema Kwa nini tujitoe katika utungwaji wa katiba wakati hatujajadili ibara hata moja ya katiba ambayo ina ibara 171 ya katiba? 
 (3). Alisema hakuna jukwaa kubwa la kusikilizwa na watanzania wote duniani zaidi ya hili jukwaa la katiba ambalo linasikilizwa dunia nzima kwa hivyo kama kuna hoja za msingi tuzisemee hapa. 
(4). Kwa mujibu wa kanuni sisi tumetengewa saa 6 hivi ni kweli hatuwezi kuwajibu hawa CCM na tuna dakika kumi kumi kweli? tutashindwa kuzitumia kuwajibu hawa na kuvuruga hoja zao? 
(5)Tusikimbie vita tupigane hapa hapa. Lakini mwisho alisema waheshimiwa wajumbe kama mnataka tuondoke mimi nipo tayari kuondoka lakini nitaondoka kwa kuwa wenzangu wameamua kuondoka lakini nitaondoka hali ya kuwa najua tunavunja bunge tukiwa na hoja dhaifu.

Comments

Popular posts from this blog