Rais Kikwete Alipowasili Viwanja vya Bunge Dodoma na kukagua Bwaride Maalum.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Samuel John Sita akibadilishana mawazo na
Makamu Mwenyekiti wake nje wa Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma kabla ya
Kuanza kwa uzinduzi wa Bunge Maalum uliofanywa na Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.kushoto Katibu wacBunge
Maalum Yahya Hamad Khamis.
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiingia
ndani ya Viwanja vya Bunge kulihutubia Bunge Maalum la Katiba Mjini
Dodoma leo.
Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akikagua gwaride rasmi lililotayarishwa na Jeshi la Polisi kabla
ya kuzindua Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR )
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibnar
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amesema Umma
wa Watanzania utajaa matumaini endapo jukumu walilopewa wajumbe wa
Bunge Maalum la Katiba watalizingatia vizuri na kulithamini ipasavyo.
Alisema
jukumu hilo litaweza kufanikiwa vyema kama wajumbe hao watazingatia
ipasavyo misingi ya utulivu, hekima, na busara wakati wa kujadili rasimu
ya Katiba ya pili iliyopo mikononi mwao hivi sasa.
Dr.
Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na Wabunge wa Bunge Maalum
kwenye uzinduzi rasmi wa Bunge hilo Maalum la Katiba linaloendelea Mjini
Dodoma lilijumuisha Wawakilishi zaidi ya Mia 620 kutoka vyama vya
siasa,Taasisi na Jumuiya tofauti za Kijamii.
Alifahamisha
kwamba kazi ya wajumbe hao wa Bunge Maalum la Katiba ni kujadili,
kuamua na hatimae kutunga katiba Mpya inayosubiriwa na Wananachi kwa
ajili ya kuitolea maamuzi.
“
Fursa ya Utungaji wa Katiba mliyoipata Mkiipatia Tanzania Katiba Mpya
bila shaka Historia itawaandika kwa wino wa dhahabu hasa mkitunga Katiba
itakayotekelezeka na kuondoa changa moto zilizopo kwa pande zote mbili
za Muungano “. Alisisitiza Rais Kikwete.
“
Hamna budi kujidhirisha juu ya vifungu kwa vifungu vya rasimu, neno kwa
neno, Sentensi jkwa sentensi ili mfikie pahali kwa kujidhihirisha.
Tunachotaka Watanzania kupata Katiba iliyo bora, Vyenginevyo tutakua na
katiba itakayokujahitaji kutengenezwa tena haliambayo si rahisi “.
Aliendelea kufafanua Dr. Kikwete.
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alieleza kwamba Demokrasia ndani ya
Tanzania imestawi na kujenga mizizi kwa vile wananachi walio wengi wako
wazi kutoa maoni na mawazo yao kwa uhuru mpana zaidi.
Alifahamisha
kuwa madai ya Tanzania kuwa na Katiba Mpya yalianza kuibuka ndani ya
mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa nchini na kupelekea kufikia hatua ya
kuanzishwa kwa mchakato wa kutunga katiba mpya alioamua kuutangaza
rasmi Tarehe 31 Disemba mwaka 2010.
Amewataka
wajumbe hao kuwa makini katika kuyapitia kwa kina mapendekezo ya
yaliyomo ndani ya rasimu hiyo kwa vile mengi yamekuwa katika utaratibu
mpya ili kuepuka kabisa mwanzo wa Katiba hiyo kushindwa kurekelezeka.
Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete alifafanua kwamba mfumo wa Serikali mbili ulipo
hivi sasa hauna mashaka katika kutekelezeaka lakini kazi ya Wajumbe hao
wa Bunge Maalum la Katiba ndio itakayosubiriwa na Wananachi katika kutoa
Maamuzi.
Alisema
kitakachohitajika kwa wakati ujao na kwa Viongozi hao kujenga hoja na
ushawishi utakayowaridhisha wananchi kukubali mfumo wa Katiba
watakayopendekeza.
Akizungumzia
suala la muundo wa Serikali ya Muungano Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
aliwatahadharisha wajumbe hao wa Bunge Maalum la Katiba kuwa makini
katika maamuzi ya mfumo utakaowaletea tija Wananchi wa pande zote Mbili.
Dr.
Kikwete aliwaasa kwamba maamuzi yasio sahihi katika mfumo wa muundo huo
ama kuwa wa Serikali Mbili au Tatu unaweza ukaitia hasara kubwa nay a
muda mrefu Nchi.
Uzinduzi
huo wa Bunge Maalum la Katiba la Muungano umeshuhudiwa pia na Viongozi
Mashuhuri wa Kitaifa, Wawakilishi wa Taasisi na Mashirika ya Kimataifa
wapatao 52 , Viongozi wasataafu wa Serikali zote mbili za SMT na SMZ
pamoja na Wakuu wa Vikosi vya ulinzi na Usalama Muungano na Vile vya
SMZ.
Mapema
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
alipokea saluti iliyoandaliwa rasmi Kabla ya uzinduzi wa Bunge hilo
kutoka kwa Jeshi la Polisi pamoja na kuimbwa wimbo wa Taifa wa Serikali
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba tayari wameshatunga Kanuni za Bunge Maalum za
Mwaka 2014 chini ya Kifungu cha 26 {1} cha Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Sura ya 83.
Comments
Post a Comment