RAIS BARACK OBAMA AKUTANA NA PAPA FRANCIS KWA MARA YA KWANZA VATICAN


Rais wa Marekani,  Barack Obama akiwasiri Vatican kwa ajili ya mazungumzo na Papa Francis kwenye mji wa Vatican jana march 27, 2014.
 


 Rais wa Marekani, Barack Obama akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili Vatican

  Rais wa Marekani, Barack Obamaakisalimiana na mmoja wa padri Georg Ganswein alipowasili Vatican


 Papa Francis akutana na Obama

Rais Obama ameelezea furaha yake ya kukutana na papa mtu ambaye kulingana naye anaishi na kutenda kulingana na injili anayoihubiri.


Maswala mbali mbali yenye umuhimu wa kimataifa pamoja na kidini huenda yakajadiliwa katika mkutano huo. Wawili hao wanatarajiwa kujadili namna ya kupunguza tofauti iliyopo kati yao katika maswala mengi mbali na kujaribu kuinua maisha ya watu maskini duniani.


Papa Francis amekuwa mstari wa mbele akipigania kubadili sera na mtazamo wa Kanisa na viongozi duniani kuhusiana na mikakati ya kupunguza tofauti kubwa baina ya maskini na matajiri duniani. Aidha viongozi hao wawili wanatazamiwa kujadili hali ilivyo nchini Ukraine, na suala la upatikanaji wa amani Mashariki ya Kati.


Muafaka baina ya mitazamo tata ya wawili hao kuhusiana na maswala ya uavyaji mimba, matumizi ya dawa za kupanga uzazi na ndoa ya jinsia moja pia inatarajiwa kuwa kati ya mada itakayojadiliwa. Baada ya kukutana na papa, Obama ameratibiwa kukutana na rais wa Italia Giorgio Napolitano mbali na waziri wake mkuu Matteo Renzi.



Obama amezuru Roma baada ya siku tatu ya mazungumzo na viongozi wa Uholanzi na Umoja wa ulaya huko Brussels ambapo mada kuu ilikuwa ni taharuki inayokumba eneo zima la Crimea na Ukraine




Picha na Yahoo, Maelezo na BBC Swahili

Comments

Popular posts from this blog