MWENYEKITI WA CHADEMA AHAMIA CCM ... ATOA MAZITO YA MOYONI IKIWEMO YA KUIMALIZA KABISA CHADEMA KALENGA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kata ya Nzi akijitambulisha Rasmi kwa Wananchi wa Kijiji cha Nzi kuwa yeye 
ameamua kuachana na Chadema na Kujiunga na CCM kwa hiari yake baada ya kupima Uwezo wa Chadema na CCM kwenye Hoja na Matendo.Mwanachama huyu Mpya wa CCM ameahidi kuongoza timu ya Ushindi kwenye Kata ya Nzi kuhakikisha Godfrey Mgimwa napita kuwa Mbunge.
Pia amesema ataiweka wazi mipango ya Chadema na Watu wageni wa Chadema waliokodishwa na Kupangishwa Nyumba kata ya Nzi wanaotembea Usiku kwaajili ya Kutafuta kura na kushambulia Waoaunga mkono CCM kwenye kata ya Nzi.
Aliyekuwa Mwanachama wa Chadema kutoka kijiji cha Kamiyu na Katibu Mwenezi wa Chadema kata ya Kamiyu akitangaza kuachana na Chadema na Kujiunga na CCM hii leo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Nzi.

Comments

Popular posts from this blog