MOTO WA AJABU WAMUUNGUZA SEHEMU ZA SIRI

Doto Omari kushoto aliyeunguzwa na moto wa ajabu sehemu za siri.
Na Chande Abdallah 
KATIKA tukio linalohusishwa na ushirikina, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Doto Omari (30, pichani) ameunguzwa na moto wa ajabu sehemu zake za siri.
Moja ya jeraha alilolipata.
Tukio hilo la aina yake lilitokea alfajiri ya Machi 16 mwaka huu,   Mwananyamala – Kichangani, Dar,  wakati mwanamke huyo alipokwenda chooni kujisaidia.
Akizungumza na waandishi wetu, Doto alisema alipoanza kujisaidia, alishangaa kuona moto mkubwa ukitokea ndani ya shimo la choo na kumuunguza sehemu zake za siri, jambo lililomfanya apige kelele kuomba msaada.
“Yaani ule moto ulikuwa mkubwa halafu wa kijani huku ukiwa na muungurumo wa ajabu. Mimi nilishangaa kuuona ukinifuata na kuniunguza,” alisema.
Kaka wa mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Adam, alisema aliposikia kelele za moto, alikimbilia maji akijua ni wa kawaida.
“Mpaka sasa tumechanganyikiwa sana, hilo siyo tukio la kwanza, yako mengi, nilishawahi kumuona mtu wa ajabu  kainama kwenye mlango wa kuingilia chooni halafu kufumba na kufumbua akapotea, hii nyumba siyo kabisa.
 “Wengi ukiwaambia jambo hili huona kama hadithi, lakini matukio ya aina hii hapa Kichangani ni jambo la kawaida sema watu wanaogopa kusema,” alisema Adam.
Naye wifi yake Doto aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema aliona moshi mweusi ukitokea chooni huku kukiwa na harufu ya kama kitu kinachoungua, ingawa hakuuona moto zaidi ya kumuona wifiye akigaragara chini akidai kuungua.
Hadi waandishi wetu wanaondoka eneo la tukio, ndugu hao walikuwa wakijiandaa kumpeleka Doto kwa mganga wa kienyeji maeneo ya Lugoba, Chalinze kwa matibabu.SOURCE GPL

Comments

Popular posts from this blog