Mjamzito Ajifungua Akiwa Ndani ya Choo cha Gesti Huko Songea

WOMAN
MKAZI wa kitongoji cha Sogea katika Mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba, Pendo Lyala (18) amejifungua mtoto katika choo cha nyumba ya kulala wageni. Pendo alijifungua Machi 10 mwaka huu saa 4:00 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Kiswahili , iliyopo nyuma ya Shule ya Msingi Mwaka, mkabala na barabara kuu iendayo Sumbawanga mkoani Rukwa.
Mmoja wa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni aliyekuwa zamu, Tresia Albeto, alidai msichana huyo aliingia usiku huo na mpenzi wake aliyejiandikisha kitabuni kwa jina la Fred Gamba, mkazi wa Njombe, ambaye alikuwa amechukua chumba namba tano.
Tresia alidai mara baada ya kuoneshwa chumba hicho, Gamba alitoka nje na kuingia katika chumba hicho mara tatu katika nyakati tofauti, akiwa anamuacha mpenzi wake ndani na kuna wakati aliingia akiwa na mfuko wa plastiki (Rambo) uliokuwa na chipsi na soda.
Mhudumu huyo alisema baada ya Gamba kutoka mara ya mwisho na kwenda nje, ilisikika sauti ya kike ikiomba msaada, jambo lililomsukuma kwenda kushuhudia kilichokuwa kikiendelea.Alidai baada ya kuingia katika chumba hicho, alimkuta mwanamke huyo akiendelea kupiga kelele ya kuomba msaada akiwa katika choo cha chumba hicho.
Alidai alikwenda moja kwa moja chooni, kulikokuwa kukitokea sauti na kumkuta msichana huyo amelala chini na mtoto aliyekuwa amejifungua muda mfupi, alikuwa pembeni ya shimo la choo akilia.

Alidai kuwa kutokana na mayowe yaliyopigwa na mwanamke huyo, baadhi ya wageni waliokuwa katika nyumba hiyo, pia waliamka na kujaribu kutoa huduma ya kwanza, lakini walikwama kwa sababu ya ukosefu wa vifaa salama.
Tresia alidai hali hiyo iliwachanganya kwa kutokujua la kufanya hadi alipojitokeza msamaria, ambaye ni miongoni mwa wapangaji aliyekuwa na mke wake, alipomchukua na kumpeleka katika Kituo cha Afya Tunduma.
Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii katika mamlaka ya Mji mdogo wa Tunduma, Godfrey Simbeye alithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa msichana huyo anaendelea kupata matibabu hospitalini hapo na hali ya mtoto inaendelea vizuri.
Simbeye alidai msichana huyo alikuwa na Gamba ambaye walikutana naye usiku huo na kwamba alipokuwa chumbani, alihisi haja kubwa ndipo alipoenda chooni na wakati huohuo kujisikia uchungu.
Akizungumza katika wadi ya wazazi, Pendo alidai alishangaa kuona mtoto, kwani hakujua kama muda wa kujifungua ulikuwa umefika. Alidai kuwa Gamba walikutana kwa usiku huo na kufanya makubaliano.

Pendo alidai kuwa ni mhudumu katika baa aliyoitaja kwa jina la Udizungwa, iliyopo eneo la ofisi za CCM Kata ya Tunduma, ambako ndiko alikutana na Gamba.

Comments

Popular posts from this blog