Kupotea kwa Ndege ya Malaysia Picha zaonyesha mabaki baharini'
Serikali
ya Malaysia imesema kuwa picha mpya za Satelite zimeonyesha zaidi ya
vifaa miamoja vinavyodhaniwa kuwa mabaki ya ndege yake iliyotoweka zaidi
ya wiki mbili zilizopita.
Waziri wa
usafiri wa nchi hiyo, Hishammuddin Hussein, amesema kuwa picha hizo
zilizotolewa na Ufaransa, zinaonyesha vifaa hivyo kuwa zaidi ya mita
ishirini kwa urefu.
Hadi kufikia sasa, hakuna taarifa rasmi ya mabaki ya ndege hiyo kuonekana.
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 239, ilikuwa safarini kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Msako uliofanywa baharini na angani, kuitafuta ndege hiyo umeanza tena katika pwani ya Australia baada mawimbi kutulia baharini.
Comments
Post a Comment