HAYA NDIO MAMBO NANE(8) AMBAYO HUTAKIWI KUYASEMA KWENYE VIKAO

Kama unaingia kwenye kikao, unatakiwa uonyeshe uwezo wako wa kuchangia ili mambo yaende vizuri na kuwa bora zaidi, usiongee vitu vya kukatisha tamaa au visivyokua na tija.


1. Ngoja nikupe rejea kuhusu jambo hilo...

Rejea sio jambo baya kama ni nzuri na imefanywa vizuri inasaida kundi kupata suluhisho la jambo fulani, lakini wakati mwingi mtu akisema anataka kutoa rejea ya kitu fulani ni kujaribu kutupilia mbali maswali, kama hauko tayari kutoa suluhisho ya jambo fulani ruhusu mazungumzo yaendelee mbele na rejea hiyo kaa nayo mwenyewe.



2. Nimeshatuma Barua Pepe

Mazungumzo ya Uso kwa Uso hayatakuwa na maana kama ukisema umeshatuma barua pepe na kila mmoja akasome. Badala yake ongelea kwa muhtasari suala hilo ili kila mmoja ajue ni kitu gani kinaendelea.



3. Hilo si jambo la msingi sana.

Maneno kama hayo hutokea mara nyingi, ukisema jambo si la msingi, kwanini? Hata kama jambo linaloletwa mezani si la wakati huo haimaanishi lisichuKUliwe umaanani. Kwa mwingine kwenye kitengo chake ni jambo la muhimu sana.


 4. Hakuna anayekubaliana na Hilo

Kwenye kikao inatakiwa kila mtu atoe mchango wake na mawazo yake. Kama kuna mtu anakuja na kauli hiyo unatakiwa kuwa makini, inawezekana ni kweli au aliyekuja na kauli hiyo kuna kiTu kinaendelea ambacho wewe hukijui. Mara nyingi wazo zuri ni lile kila mtu anafikiri litashindwa vibaya. Ukiona vipi, angalia kwa ukaribu zaidi kile watu wengi wanaonyesha hawakipendi.



5. Hakuna wazo baya.

Wakati hutakiwi kukatilia mbali wazo ambalo kila mmoja halipendi, hakuna wazo baya, wazo baya huja kutoka kwa watu ambao hawakuwepo kwenye kikao. Kama utaruhusu wafanyakazi wakawa huru kutoa mawazo yao, utapunguza majadiriano yasiyokuwa ya msingi.



6. Mimi ndo kiongozi hapa

Hiyo ni kauli ya kuondoa mawazo, kutawala watu waliohudhuria kikao au unataka kurudisha mambo kwenye mstari. Hiyo inaweza kuwa taa nyekundu kwamba mtu huyo anajiona hana madaraka au kikao hicho si cha majadiliano hasa.



7. Ngoja tutafute Mtaalamu mzuri
Vikao ni kwaajili ya majadiliano, unapoongea kwamba hapo hakuna mtu mwenye ujuzi ambaye anaweza kuongea suala fulani unasababisha na kunyamazisha mjadala mahala hapo. Inawezekana una mawazo kuhusu mtu nje ya hicho kikao ila unapotoa kauli hiyo unajiweka matatani. Unakuwa ni mtu mwenye kutilia mashaka kila mtu unayefanya naye kazi.

8.Tutakuwa na Kikao cha ufuatiliaji

Hiyo ni mbaya zaidi, kwani kikao ulichopo sasa kazi yake ni nini? Ni vizuri ukisema kikao cha ufuatiliaji hakitakuwepo kwa kuwa mtu husika wa jambo hila atakuwa akitupasha haLi kwa kila kinachoendelea.
Je una mawazo yako binafsi ? Haukubaliani? Usisite kutuandikia mawazo na mchango wako.

Comments

Popular posts from this blog