ANGALIA PICHA WANAUME AUAWA KWA KUCHOMWA AKITUHUMIWA KWA U SHOGA UGANDA
Ni muda
mfupi tu toka Uganda ipitishe sharia ya kupinga ushoga, imeripotiwa mtu
mmoja aliyetuhumiwa kuwa shoga alichomwa moto mpaka kufa nchini humo.
CNN
imeripoti tukio hilo ambalo jina la mtu huyo halikuweza kujulikana.
Picha ilionesha jinsi mtu huyo anavyochomwa moto huku akiwa pembeni mwa
reli huku watoto wakishuhudia tukio hilo.
Sharia
hiyo iliyopitishwa hivi karibuni, inahusisha pamoja na kufungwa maisha
kwa mtu yoyote atakayejihusisha na shughuli zozote za ushoga pamoja na
kuambukiza ukimwi, matendo ya ngono na watoto pamoja na watu wenye
ulemavu, udhalilishaji ikiwa ni pamoja na ubakaji.
Sharia hiyo
iliyozaliwa mwaka 2009, na kupewa jina “Kill The Gays” ikimaanisha “Ua
Mashoga” ambayo ilisisitiza hukumu ya kifo kwa matendo fulani ya ushoga,
lakini ilirudishwa kabatini kutokana na kelele nyingi zilizopigwa na
mataifa mbalimbali.
Katika
sharia hii mpya, mtu yeyote atakaye fungisha ndoa ya jinsia moja
atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka 7. Atakayeshindwa kutoa taarifa ya
ushoga polisi pia ni mualifu.
Madaktari
watakao watibu mashoga, watakaopangisha mashoga kwenye nyumba zao na
wale wataka shukiwa kuwa mashoga, wasagaji, waliobadilisha jinsia na
mabasha watafungwa miaka 5.
Mtu yeyote atakayetoa msaidia kwa shoga atakuwa anavunja sharia, ambapo atachukuliwa hatua.
Watu
wengi wanaamini kuwa sharia hii ni muhimu ili kupinga tabia na tamaduni
za nchi za magharibi. “ hii sharia ni muhimu kwa nchi hii ili kulinda
tamaduni za Mwafrika” alisema David Bahati ambaye ni mbunge ambaye
aliuwakilisha muswada huo bungeni.
Bahati pia ni mmoja kati ya kundi linalotuma fedha katika nchi za Afrika kuunga mkono wanaopinga shughuli zote za ushoga.
Comments
Post a Comment