ANGALIA PICHA MWALIMU ABAMBWA AKIJIUZA,ASEMA MSHAHARA MDOGO
Mwalimu akiwa ameduwaa baada ya kunaswa kwenye sakata hilo.
Wakati
Wakristo bado wapo kwenye Kwaresma, mama aliyejitambulisha kuwa ni
mwalimu wa shule ya msingi, amenaswa laivu akijiuza maeneo ya
Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri Machi 24,
mwaka huu ambapo awali, wakazi wa eneo hilo waliwatonya mapaparazi wa
Operesheni Fichua Maovu (OFM) kuwa kuna danguro kubwa maeneo ya Kizuiani
ambalo limesheheni madadapoa wa kila aina wakiwemo mabinti wadogo.Chanzo
hicho kilimwaga data kuwa, kuna mzee maarufu kwa jina la babu katika
eneo hilo ambaye amekuwa akiwapa machangudoa hifadhi katika banda lake
na kuwapa magodoro chakavu kwa malipo ya shilingi elfu moja kwa kila
kichwa.
KISIKIE CHANZO
“Jamani kwenye danguro hili kila aina ya uchafu upo. Wanatukwaza sisi
Wakristo ambao tupo katika kipindi hiki cha Kwaresma,” kilitiririka
chanzo hicho cha kuaminika maeneo hayo.
OFM KAZINI
Ili kujiridhisha na taarifa hizo, makamanda wawili wa OFM walitimba
katika danguro hilo wakajifanya wateja ambapo walimchukua mmoja na
kubaini kuwa ni mwalimu wa shule ya msingi.
TUJIUNGE NA CHANGU MWALIMU
“Kaka ongea fasta nipe changu, usinione hivi mimi ni mwalimu wa
msingi, mshahara haukidhi halafu isitoshe serikali haijatulipa
malimbikizo yetu, watulipe bwana pengine tunaweza kujikwamua,” alisema
changu huyo ambaye alimtaka kamanda wa OFM alipie shilingi elfu kumi
kama malipo ya huduma tendo moja.
POLISI WAITWA
Baada ya kujiridhisha kwa uwepo wa biashara hiyo, OFM waliwapigia
simu polisi wa Kituo cha Kizuiani, wakafika na kufanikisha zoezi la
kuwakamata machangu wapatao 16 pamoja na babu anayewapa hifadhi ili
wauze miili.
VIBANDA KIBAO VYABAINIKA
Wakati zoezi la kuwakamata likiendelea maeneo hayo, vilibainika
vibanda vingi ambavyo machangu hao hufanyia uchafu wao pamoja na mfuko
mkubwa ambao madadapoa hao huhifadhia nguo zao za heshima kabla
hawajaingia ‘mzigoni’.
WAACHA WATOTO NYUMBANI
Baadhi ya machangudoa hao waliotiwa mikononi mwa polisi, walikiri
kuwa wamewaacha watoto wao nyumbani huku wengine wakidai ni wake za watu
hivyo kuomba wasipigwe picha kukwepa aibu pindi zitakapochapishwa
gazetini.
“Jamani msitupige picha sisi wengine tuna watoto na waume zetu, tunaomba msamaha jamani,” walisikika madadapoa hao.
WAFIKISHWA POLISI
Baada ya kamatakamata kukamilika, machangu hao pamoja na mzee huyo
walipandishwa kwenye difenda la polisi na kupelekwa katika Kituo cha
Polisi Kizuiani kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa
Mahakama ya Jiji kujibu mashitaka ya uzururaji.
SOURCE:GPL
Comments
Post a Comment