ANGALIA PICHA MKE WA MTU AFUMANIWA AKINGONOKA NA SHEMEJI YAKE
Ujira wa usaliti ni aibu kubwa! Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Baba Anorld almaarufu Ngosha, amedai kumfumania laivu mkewe, Anjela ‘Mama Anorld’ akiwa chumbani na shemeji yake aliyetajwa kwa jina moja la Paulo.
Tanganyika jeki: Mtuhumiwa Paulo akiwa kakamatwa Tanganyika jeki baada ya kunaswa.
Fumanizi hilo lilitokea usiku wa kuamkia
Jumatano wiki hii, nyumbani kwa wanandoa hao huko
Vingunguti-Mikoroshoni, Dar baada ya Ngosha kumwekea mkewe huyo mtego.
Ilielezwa kuwa awali, Ngosha alikuwa
akishirikiana na Paulo kwa mambo mengi na hakuwa na shaka naye lakini
kuna siku moja majirani walimwambia ‘Oyaaa…babu shtuka mali zako
zinaliwa, tena kikulacho ki nguoni mwako’.
Ilielezwa kuwa baada ya kuambiwa maneno
hayo alitafakari lakini akashindwa kupata majibu hadi pale alipotamkiwa
kabisa kuwa jamaa yake anamsaliti kwa mkewe.
Ngosha alisema katika uchunguzi wake,
wapambe walimng’ata sikio kuwa anazungukwa na Paulo ambaye amekuwa
akimuita mama Anord shemeji huku akimng’ong’a Ngosha kisogoni.
Ilisemekana kuwa wapambe hao walimtonya Ngosha kuwa akiwa hayupo mgoni huyo na mkewe huingia chumbani kwake na kufanya yao.
MTEGO WATEGWA, OFM MZIGONI
Habari zilieleza kuwa baada ya ‘kujazwa
sumu’ juu ya taarifa hizo, Ngosha aliwaomba wapambe hao wamsaidie kutega
mtego huku Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ikiomba
kuingia mzigoni.
ILIKUWAJE?
Ngosha aliambiwa ajifanye amesafiri na kutarajia kurudi kesho yake.
Akiwa kazini, alimpigia simu mkewe
akamtaarifu kwamba asimuandalie chakula kwa kuwa kuna ‘kijisafari’ cha
dharura na kutarajia kurudi kesho yake.
Ngosha hakusafiri, badala yake alikuwa
mtaa wa pili huku mashushushu wake wakilizunguka eneo la tukio na
kuangalia kila kilichokuwa kikiendelea kisha kutoa taarifa kwake.
PAULO AWASILI KWA MBWEMBWE
Ilipofika saa 3:43 usiku, Paulo aliwasili
eneo la tukio na kuingia chumbani kwa Ngosha akiwa na kifurushi chenye
chipsi na vipapatio vya kuku.
Bila kujua nje kuna wapigachabo
waliopandikizwa na Ngosha, wawili hao walianza kupiga stori za
‘Kivalentine’s Day’ wakijua mwenye ndoa yake alikuwa safarini.
‘TAP’ TAA YAZIMWA
Kwa mujibu wa wapigachabo hao, saa 6:12
usiku, yale mazungumzo yalikatika ambapo wawili hao walizima taa ndipo
mashushushu walipomtaarifu Ngosha.
NGOSHA ARUKIA MLANGO
Saa 6:14 usiku, Ngosha alipokea simu
kutoka kwa wapigachabo wake waliomtaarifu kuwa tayari mambo ‘yamekwiva’
chumbani kwake na ndipo mwenye mali huyo alipokimbilia eno la tukio.
Alipofika aliurukia ‘samasoti’ mlango wa mninga ambao ulimdindia na kukataa kuvunjika.
Ngosha, akiwa kwenye tafakuri kuntu ya
namna ya kuvunja mlango, baba mwenye nyumba aliyejitambulisha kwa jina
moja la Ndosi alitokea na kumdhibiti huku akimsihi asifanye vurugu wala
kuua mtu bali ajaribu kuwagongea kiustaarabu ili kuunusuru mlango wake.
WAVAA CHAPUCHAPU
Saa 6:21 usiku, wakati wakigongewa
walitumia nafasi hiyo kuvaa chapuchapu na kufungua mlango wenyewe ambapo
liliibuka varangati zito kati ya wawili hao walionaswa na Ngosha na
kundi lake ambapo palichimbika.
Kitendo cha kumfumania mkewe laivu kilimfanya Ngosha amwage chozi la kiutu umzima kutokana na kutoamini alichokishuhudia.
MGONI APIGWA FAINI
Saa 6:45 usiku, ingawa varangati lilikuwa
kubwa lakini wasamaria wema waliingilia kati na kuwatuliza kisha
kuwataka Ngosha na mgoni wake (Paulo) wakae kitako na kuyazungumza kiutu
uzima kwa maana hata Rich Mavoco ameimba kwenye Wimbo wa Roho Yangu
kuwa ‘ku….. ni siri ya ndani’ hivyo nao walifanye jambo hilo liwe siri.
Paulo na Angela waliwekwa kitako na
wasamaria wema pamoja na mwenye mke na kujadiliana jinsi ya kufanya
ambapo awali Paulo alisema atampa Ngosha faini ya Sh. milioni moja ili
yaishe.
Wakati Ngosha akijiandaa kupokea kitita
chake, alishangaa Paulo alipomuambia fedha hiyo waandikishiane
kimaandishi kwa kuwa hakuwa nayo mkononi.
Ngosha aliona longolongo na kuomba msaada wa wasamaria wema wamsaidie kuwafikisha watuhumiwa wake polisi.
WAGONI WAPELEKWA POLISI MSOBEMSOBE
Mishale ya saa 7:42 usiku, wagoni hao
walitembezwa mtaani wakipelekwa kituo cha polisi ambapo ilipofikia saa
8:34 usiku, walikuwa wamefikishwa Kituo Kidogo cha Polisi cha Buguruni
Kwamnyamani, Dar.
Wakiwa kituoni hapo, baba mwenye nyumba
wao alitoa lake la moyoni na kuwakabidhi wote waliofumaniana kituoni
hapo na kujivua lawama.
Hata hivyo, hadi OFM inaondoka kituoni hapo, bado wahusika walikuwa wakihojiwa ili sheria ichukue mkondo wake.
Comments
Post a Comment