AFANDE SELE AKILI KUMWAGANA NA MAMA TUNDA,

SIKU chache baada ya kuzagaa kwa taarifa za kuachana na mkewe mama Tunda, mfalme wa Rhymes, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ ameibuka na kusimulia mambo ya kusikitisha waliyopita katika safari ya maisha yao.

Mfalme wa Rhymes, Seleman Msindi ‘Afande Sele’.
Akizungumza na wanahabari wetu ndani ya Ukumbi wa Meeda, Sinza-Mori, Dar, juzi Afande alisema hadi kufikia hatua ya yeye kutangaza kuwa ameachana na mama Tunda ambaye amedumu naye kama mume na mke kwa zaidi ya miaka 10, alikuwa akivumilia mambo mengi na mwisho kuamua kuachia ngazi.


Afande Sele akiwa na familia yake.
“Nilikuwa nikielezwa mengi kuhusu mke wangu, nilishapigiwa simu na kuambiwa mke wangu anagombaniwa na wanaume usiku klabu lakini huwa mimi siyo mtu wa kuishi kwa hisia, nilivumilia nikiamini atajirekebisha, haikuwa hivyo.
“Japo sikuwa na uthibitisho wa moja kwa moja, lakini nyumbani alikuwa siyo mtu wa kutulia, amekuwa akinizunguka hadi kwa washkaji zangu wa karibu. Kuna jamaa alichoshwa na habari hizo akanifuata na kuniambia hata kama lakini uvumilivu wangu ulizidi,” alisema Afande kwa hisia.
Akiendelea kushusha masikitiko yake mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, Afande alienda mbele zaidi kwa kusema mbali na mkewe huyo kumsaliti kwa wanaume tofauti wakiwema marafiki zake, ilifika wakati mama Tunda akawa anachukua fedha ndani na kwenda kutumia na wanaume.
Alisema alitumia mwanya wa mkali huyo wa mashairi anapokuwa amesafiri katika shoo mbalimbali na kuachiwa fedha za matumizi pamoja na ujenzi wa nyumba yao mpya, kutanulia.

“We acha tu, yaani fedha za matumizi, ujenzi nilikuwa namuachia lakini cha kusikitisha ni kwamba alizitumia kutanulia, jambo ambalo nililizidi kunitia umaskini na machungu ukizingatia jamii inaniheshimu kama msanii, mbaya zaidi wananchi wamenitaka nigombee ubunge Morogoro Mjini,” alisema Afande.
Akizidi kushusha ‘vesi’, Afande alitiririka kuwa kuna wakati aliwahi kupewa taarifa na rafiki yake mwingine aishie Kurasini jijini Dar ambaye alilamika juu ya mkewe kufika kwa jamaa huyo na kuazima fedha bila kuzilipa.

Kwenye aya nyingine, mkali huyo alisema anakumbuka jinsi alivyoishi na familia yake, mkewe, wanaye Tunda na Ahsante Sanaa lakini hana jinsi kwani ameona bora kuachana kwani umri wake una mruhusu kuoa mke mwingine siku ikitokea.
“Nakumbuka maisha kidogo ya furaha na familia, mama Tunda atabaki kuwa mama wa watoto wangu lakini kamwe hawezi kurudi kwangu kwani itakuwa ni aibu juu ya aibu,” alisema.
Afande aliachana na mama Tunda mwishoni mwa mwaka jana alipotimba jijini Dar katika shughuli zake za kikazi na kumuachia mkewe fedha za ujenzi lakini aliporejea nyumbani Morogoro, alikuta mzazi mwenzake huyo ameondoka nyumbani na kuacha funguo, kila alipompigia simu hakupokea.

Alipoulizwa kuhusiana na shutuma zilizoporomoshwa na Afande, mama Tunda alitiririka:
“Alinipa Sh. milioni 3 za shoo tu, tukanunua vifaa vya ujenzi lakini siyo kwamba nilitanua na wanaume, tena kama ni kumfumania, mimi ndiye nilimkuta na mwanamke alitoka naye Fiesta Dodoma, sikutaka tu kumsema, hizo taarifa anazusha tu.

“Kwanza kuna mambo mengi tu amenifanyia, alikuwa mlevi kwani hadi wazazi wangu walikuwa wakinishangaa sana, sasa na mimi nikaona bora niachane naye,” alisema mama Tunda.

Comments

Popular posts from this blog