Wanasayansi wa kampuni ya Google: Wabuni magari yasiyotumia dereva Jionee

 

Inawezekana kuwa na magari yasiyokuwa na dereva? Kampuni ya mawasiliano ya kompyuta ya Google inasema ndiyo. Magari hayo yapo na yataongozwa kwa kutumia kompyuta pekee, huku yakiwa na uwezo mkubwa wa kuepuka au kutosababisha ajali barabarani.

Wanasayansi wa Google wanaosimamia teknolojia hiyo mpya, wanaamini kwamba madereva wanafanya makosa mengi wawapo barabarani, yakiwepo ya kizembe ama bahati mbaya na ndiyo yanakuwa chanzo cha ajali mbaya barabarani.
Wakati teknolojia ya kompyuta ilipogundulika, wanasayansi walisema wamegundua mbinu ya kufuta makosa ya kibinadamu katika shughuli za hesabu.
Waliamini kuwa kila hesabu 500 afanyazo mtu ambaye ni mtaalamu wa fani hiyo, lazima kuwepo na makosa yasiyopungua mawili. Lakini baada ya kugundua kompyuta, maelfu kwa maelfu ya hesabu yanaweza kufanyika bila makosa.
Makosa hayo ya kibinadamu yanayoweza kufanywa na mtu bila kukusudia, ndiyo yanayoaminika kuweza kufanywa na dereva yeyote akiwa barabarani.
Magari hayo yako je?
Mtaalamu wa kompyuta katika Chuo Kikuu cha Stanford, Profesa Sebastian Thrun, anayesimamia, teknolojia hiyo akisaidiana na mhandisi wa kampuni ya Google, Chris Urmson, wanasema teknolojia hiyo itasaidia kuepusha ajali, foleni na pia kupunguza kiwango cha mafuta yanayopotea kutokana na uendeshaji usiofaa.
Mhandisi Urmson anasema magari hayo hayatakuwa na tofauti kwa kiasi kikubwa na mwonekano au miundo ya magari yaliyopo sasa. Kama haitoshi yana chaguo la ama liendeshwe kwa kompyuta ama na dereva.
Mwonekano wake
Kimwonekano, magari hayo anayaelezea yatatofautiana na mengine, kwa kuwa na kifaa maalumu juu ambacho kinasaidia mawasiliano na kutambua maeneo.
Anasema kwenye mfumo wa kompyuta zitatumika programu mbalimbali kama vile ya 3D, ambayo itasaidia kuliongoza gari kulingana na ramani ya eneo.

“Hii ina maana kwamba magari yote yatakuwa yanatumia ramani ambayo lazima iingizwe kwenye mfumo wake ili itambue barabara itakazopita ili kufika aneo ambalo mhusika ama wahusika wanataka” anasema.

Comments

Popular posts from this blog