MWANAUME ANAYEWEZA KUKAANGA KUKU KWENYE MAFUTA KWA MIKONO YAKE BILA KUUNGUA
Mwanaume huyo (52) mkazi wa jiji la Chiang Mai ambaye ni mpishi huko Thailand, ana uwezo wa ajabu wa kuzamisha mikono yake katika mafuta yenye moto wa digrii 480 bila kuungua na amedai kuwa huwa hasikii maumivu ya aina yoyote wala ngozi ya mikono yake haidhuriki na mafuta ya moto mkali.
Mr Trichan anashikilia rekodi ya dunia kwa kukaanga vipande 20 vya kuku katika mafuta ya moto wa 480c ndani ya dakika 1.
Kutokana na maajabu hayo ya mikono yake mwanaume huyo amepata umaarufu wa kimatifa uliompa faida zaidi katika biashara yake kwani watu mbalimbali kutoka pande tofauti za dunia wamekuwa wakitembelea ofisi yake ya chakula “Fried Chicken Iron Hands Man” ili kushuhudia jinsi Kann anavyoweza kutumia mikono yake kuchota kuku kutoka kwenye mafuta ya moto.
Mwanaume huyo na mke wake wamekuwa wakisafiri duniani kuonesha maajabu hayo ambayo hajui ni jinsi gani ameweza kufanya anachokifanya na mikono yake, lakini anafuraha sababu inamuongezea wateja zaidi katika biashara yake kila siku.
Mr Trichan aligundua kipaji chake hicho cha kipekee miaka nane iliyopita baada ya kumwagikiwa na mafuta ya moto kwa bahati mbaya lakini hakudhurika.
Onyo: Usijaribu hii nyumbani.
Comments
Post a Comment