Majibu ya Msanii Linah Kuhusu tetesi za Yeye Kuwa Mama Kijacho

Muimbaji wa THT, Linah Sanga amesema tetesi za kuwa ni mjamzito si za kweli.
Linah ameiambia Mdadisi Mambo blog kuwa masuala ya ujauzito, kuolewa na kuwa na familia ni ya muhimu kwa kila msichana lakini kwa sasa bado hajaweza kuvifanya hivyo.
“Hakuna kitu kama hicho na wala hakijawahi kutokea kitu kama hicho,” Linah amesema kujibu swali kama kweli ni mjamzito.

“Mipango ipo lakini unajua mimi ni mtoto wa kike na mipango kama hiyo lazima iwepo. Nikiwa kama mtoto wa kike, nitahitaji familia, vitu kama hivyo ntavihitaji apart from kazi yangu, hata hayo masuala ya mimba na kila kitu, kuzaa na nini, ntakuwa tayari endapo Mungu atanisaidia mume, ndoa. Kwahiyo hayo yote sijui kuonekana ni maneno tu, rumors haziishi, kwa msanii kama mimi lazima rumors ziwepo, lazima watu wataongea vitu vingi vya tofauti. Hayo mambo ya ujauzito walishaongea sana lakini mwisho wa siku wanaishia kunyamaza kwasababu hakuna mtu mwenye uhakika wa hicho kitu,” amesema Linah.

Kuhusu ukimya wake, Linah amesema kwa sasa bado hajaamua ni wimbo wa kuutoa kwakuwa hataki kuwaangusha mashabiki wake.

“Sio kwamba sina nyimbo za kutoa, ninazo nyingi lakini kila ninavyoendelea kutengeneza nyimbo, navyoitengeneza ya pili inakuwa nzuri zaidi na ya kwanza, nikitengeneza ya tatu inakuwa nzuri zaidi na ya pili. Kwahiyo ni bora niwe na nyimbo nyingi niweze kuwa na choice ya kuchagua nyimbo nzuri.”Linah amesema anapenda pia kuendelea kuwapa mashabiki wake ladha ya nyimbo za taratibu ambazo wengi walimzoea tangu mwanzo

Comments

Popular posts from this blog