KUJISIKIA KICHEFU CHEFU NA KUTAPIKA WAKATI WA UJAUZITO/(MORNING SICKNESS)


Nusu ya wana wakewote wajawazito hupatwa na
tatizo la kujisikia kichefuchefu na kutapika, ni moja wapo ya dalili kuu za
ujauzito.

Husababishwa na
kuongezeka kwa hormone mwilini, maranyingi huanza katika wiki ya
sita ya ujauzito na huweza kutokea muda wowote wa siku.
Madaktari wengine huwa wa na amini ya kuwa ni dalili nzuri kwani
humaanisha ya kuwa placenta inafanya kazi
vizuri.


Kwa wanawake wengine
tatizo hili huisha katika wiki ya kumi na mbili ya ujauzito.
Lakini kwa wengine huweza kuendelea kwa kipindi kizima cha ujauzito.
Mara nyingi ni kitu cha kawaida ambacho kina kuja na kuondoka
lakini pale ambapo mama anatapika kupita kiasi
mpaka anashindwa kubakisha chakula au maji mwilini basi anahitaji kumuona daktari .
Kula milo mingi midogo mara kwa mara badala ya kula milo mikuu mitatu kwa
siku. Hii itasaidia kwa sababu wakati mwingine tatizo hili
linasababishwa na kutokuwa na sukari ya kutosha kwenye damu
(lowbloodpressure).

Sukari hii ndio chanzo cha nguvu mwilini.Ukila mara
kwa mara chakula kitapokelewa mwilini
na kutengenezwa sukari na mwili kuwa na nguvu ya kutosha.
Kunywa vinywaji nusu saa kabla au baada ya chakula.
Usinywe vinywaji na kula chakula kwa wakati mmoja.
Kula mkate wa kukausha au matunda
yaliyo kaushwa dakika 15 kabla ya kumka asubuhi.
Kunywa maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji (dehydradtion).
Jaribu kunywa litre 2.5 kwa siku ikiwa pamoja na maji, chai
au juice natural zisizo na sukari ya kuongeza.
Jitahidi usile au kupita sehemu zenye harufu ya chakula zinazozidisha tatizo hili.

Pumzika vya kutosha Napata usingizi wa mchana.
Usikae sehemu zenye joto jaribu kukaa ndani kwenye feni au nje sehemu zenye upepo.
Kwa sababu joto huzidisha tatizo hili.
Pia usiende sehemu zenye watu wengi.

Ndimu, tangawizi zinasaidia,
pia unaweza kunywa maji ya ndimu au kula tunda la tikiti maji (watermelon)

kupunguza kichefu chefu.
.Kula viazi vya kukausha na chumvi.

 
 .Fanya mazoezi.
.Usilale baada ya mlo
.Usiache kula
.Usile au kupika vyakula vyenye pili pili(spicy) au mafuta mengi.
.Usinywe kahawa au vinywajivikali
 
.Kula vyakula vya protein kabla ya kwenda kulala usiku
.Fungua madirisha au Tembea nje ilikupata
upepo na oxygen ya kutosha.
.Weka kijiko kimoja cha maji ya Apple Cider Vinegar kwenye sounces ya 
maji ya uvuguvugu kasha kunywa asubuhi kabla ya kuamka.
.Kunywa chai za Ras berry leaf, Spear mint/peppermint,
Aniseseed, Fennelseed kabla ya kuamka asubuhi.

Umwone daktari kama: Una tapika kupita kiasi

Comments

Popular posts from this blog