ICC KUAMUA HATIMA YA KESI YA KENYATTA
Mahakimu wa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa ICC mjini The Hauge, wanatarajia kuchukua uwamuzi muhimu Jumatano kuhusiana na hatima ya kesi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Kikao kimeitishwa kutokana na ombi la waendesha mashtaka kutaka muda zaidi ili kuweza kufanya uchunguzi huku mawakili wa Rais Kenyatta kutaka kesi itupiliwe mbali.
Bi Bensouda anatarajiwa kuomba muda zaidi ili kupata mashahidi wepya na ushadidi katika kesi yake dhidi ya Rais Kenyatta kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu kutokana na jukumu lake katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.
Kwa upande wao mawakili wa Rais Kenyata wakiongozwa na Bw Stephen Kay watawaomba majaji kufutilia mbali kesi hiyo kwa misingi kwamba waendesha mashtaka hawana ushahidi wa kutosha kumpata na hatia mteja wao.
Mahakimu watasikiliza hoja kutoka pande zote na kuchukua uwamuzi wao.
Akihudhuria mkutano wea viongozi wa Umoja wa afrika mjini Addis Abba wiki iliyopita rais Kenyatta aliupongeza umoja huo kwa kuiunga mkono serikali ya kenya katika kesi zake mbele ya ICC, na kupelekea jambo ambalo halijawahi kufanyika, kutathmini kanuni na utaratibu wa Mkataba wa Rome.
CHANZO:VOA
Comments
Post a Comment