HUYU NDIYE MTOTO ALIYEWASHANGAZA WANA SAYANSI DUNIANI KOTE
Wanasayansi na madaktari nchini Urusi wamestaajabishwa na mtoto mwenye umri wa miezi tisa ambaye mwili wake umekuwa ukitoa maandishi katika lugha ya kiarabu yakinukuu vipande vya maneno katika Quran.
Mtoto Ali Yakubov mwenye umri wa miezi tisa amepata umaarufu mkubwa na amekuwa gumzo dunia nzima baada ya taarifa za miujiza yake ambapo maneno tofauti tofauti ya kiarabu kuanza kutokea kwenye mwili wake.
Maandishi ya kiarabu yanayonukuu aya za Quran yamekuwa yakitokea kwenye mikono yake, miguu na tumboni na kisha kutoweka baada ya siku kadhaa na kisha maandishi mengine ya kiarabu yanayonukuu vipande tofauti vya aya za Quran hujitokeza upya.
Madaktari nchini Urusi hadi leo bado hawajui nini kinaendelea kwenye mwili wa mtoto huyo ambaye maandishi ya kwanza ya kiarabu yanayosema neno "Allah" yalijitokeza kwenye kidevu chake ndani ya wiki moja baada ya kuzaliwa.
Comments
Post a Comment